Home

Wednesday, July 13, 2011

Bebe na Cece Winans waachilia nyimbo yao Mpya


Bebe kulia akiwa na Cece
Wanamuziki mahiri wa Muziki wa Injili nchini Marekani watokao kwenye familia moja Bebe Winans na dadaye Cece Winans, wameachilia nyimbo yao mpya iitwayo “CLOSE TO YOU” ambayo imo katika album yao mpya inayotarajia kuwa gumzo katika vyombo mbalimbali vya habari na katika chati za muziki wa injili nchini humo na duniani kwa kote.

Bebe ambaye jina lake halisi anaitwa Benjamin Winans, ni mtoto wa saba kuzaliwa wakati Pricilla Winans(Cece) ni mtoto wa nane kuzaliwa kati ya watoto kumi toka katika familia yao ambayo wote ni wanamuziki wa nyimbo za injili.

Bebe na Cece tayari wamesharekodi Video ya nyimbo hiyo na Hosanna Inc imepata nafasi ya kuiona.Bebe na Cece ni moja kati wanamuziki wa injili walioanza kufanya huduma hiyo mwaka 1982 wakiwa bado wadogo.

Pamoja na kuwa Familia yao wote kuwa ni wanamuziki Bebe na Cece kwa pamoja wamekuwa wakitoa album za Muziki wa injili na wamefanikiwa kugusa mioyo ya watu wengi kwa utukufu wa Mungu.

Toka Bebe na Cece Winans waanze kuimba kwa pamoja miaka ya themanini, wamefanikiwa kutwaa tuzo tatu za Gramy pamoja tuzo mbili za Dove ambazo ni za heshima sana kwa wanamuziki wa muziki wa injili duniani kote.

Bebe na Cece Winans wakati wakishoot Video ya Close to you

No comments:

Post a Comment