Home

Tuesday, July 19, 2011

Kanisa la Eagt laanzisha mfuko wa askofu kulola


Askofu Kulola katika Moja ya Mikutano yake ya Injili
Kanisa la Evangelistic assemblies of GOD Tanzania EAGT) limekamilisha maono yake ya kuanzisha mfuko unaoitwa “EAGT MOSES KULOLA PASSION FOR THE GOSPEL”

Mfuko huu utakuwa unakusanya fedha kwa ajili ya kumsaidia Askofu Mkuu wa Kanisa hilo katika kufanya kazi ya Mungu hususani mikutano yake ya Injili ikiwa ni pamoja na kuwafikia watu wengi zaidi.

Katibu mkuu wa kanisa hilo Mch Brown Mwakipesile amesema kuwa, kazi kubwa ya mfuko huo ni kukusanya pesa zitakazosaidia kazi ya Mungu inayofanywa na Askofu kulola Mfuko huo unaosimamiwa na kanisa hilo uko huru kwa mtu yeyote mwenye mapenzi mema na nchi hii kuweza kuchangia ili kuwezesha kuwafikiwa watu wengi zaidi kwa injili ya Kristo Yesu.

Wakati wa mkutano wake uliomalizika viwanja vya jangwani jijini Dar es salaam takribani wiki tatu zimepita, mmoja wa waandaaji wa Mkutano huo unaofanyika kila mwaka na kupewa jina la The Big June Crusade Mch Florian Katunzi alisema kuwa, mwakani kupitia mfuko huu wa Moses Kulola Passion For the Gospel mahubiri yote yatakuwa yakirushwa kwa njia ya Television ili kuwawezesha watu wengi zaidi kufikiwa na Injili ya Yesu Kristo.

Mpaka sasa kanisa hilo chini limefungua akaunti maalumu katika Benki ya NBC yenye Namba 029201159921 kwa ajili ya Mfuko huo. Yeyote anayeguswa kupeleka mbele huduma ya Askofu kulola yuko huru kuchangia kupitia akaunt namba hiyo.

Askofu kulola aanaaminika kuwa ni Baba wa Injili hapa nchini amewahi kutembea kutoka Mwanza mpaka Shinyanga kwa mguu akipeleka Injili.

No comments:

Post a Comment