Home

Tuesday, July 19, 2011

Kongamano kubwa la Wanawake jijini Dar es Salaam

Mch Paul Kaisi Akiwa na mkewe Mama Debora Kaisi
Mch Paul Kaisi pamoja na mkewe mama Debora kaisi toka huduma ya LIKO TUMAINI KWA MUNGU wakishirikiana na Mama Lilian Ndegi toka LIVING WATER KAWE MAKUTI wamekuandalia Kongamano maalumu la wanawake litakalofanyika katiwa Uwanja wa sifa za Yesu ambao awali ulijulikana kama Uwanja wa Fisi ulioko manzese jijini Dar es salaam.

Katika kongamano hilo lanye kauli mbiu ya “Mwanamke ni chombo cha thamani machono pa Bwana Isaya 43:4” kutafundishwa namna ambavyo mwanamke anaweza kuwa mwombezi wa Taifa na familia  na wote walovunjika na kujeruhiwa moyo Mungu atawaponya kasha hawatabaki kama walivyo

Miongoni mwa waalimu katika kongamano hilo ni pamoja na
▪Mama Debora Kaisi
▪Mama Lilian Ndegi
▪Mama Debora Malasi
▪Mama Debora Paul Kaisi – Mwenyeji wa Kongamano

Kongamano hilo linatarajia kufanyika  Tarehe 22/07/2011 kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa kumi na moja jioni ambapo wanamuziki wa injili akiwemo Neema Mwaipopo Haika Urio Tarufaina Mbaga pamoja na Uwanja wa Sifa Praise and Worship Team watakuwa wakiimba. Wote mnakaribishwa.

No comments:

Post a Comment