Home

Thursday, July 7, 2011

Jifunze kupitia Historia ya mwanamuziki Miriam Lukindo



Miriam Lukindo
Miriam Lukindo ni Mwanamuziki wa nyimbo za injili kutoka nchini Tanzania, Miriam ambaye tofauti na uimbaji hufanya kazi za upambaji maofisini na katika matukio mbali mbali, alikulia katika jiji la mbeya ambako alikuwa akiishi yeye mama yake pamoja na bibi yake. 

Miriam alisoma shule ya msingi Kilimo Uyole na kufanikiwa kuendelea na masomo ya sekondari katika shule ya sekondari majengo iliyoko katikati ya mji wa Moshi.

Mama yake na Miriam alipata ujauzito ulipelekea kuzaliwa kwa Miriamu akiwa kidato cha Pili(form II), kwa wakati huo alikuwa na umri wa miaka kumi na sita (16) tu. Katika kipindi chote hicho toka akiwa mdogo Miriam  aliiambia Hosanna Inc kuwa alikuwa akipenda sana kuimba na alikuwa akipenda sana kusikiliza na kuimba nyimbo za Rebeka Malope.

Kwa kipindi chote hicho Miriam hakuwahi kumfahamu baba yake japokuwa aliambiwa kuwa yupo. Jambo hilo lilimuumiza na ilifikia hatua akaona ni hali ya kawaida hivyo chochote kuhusu yeye bibi yake na mama yake ndio walikuwa kila kitu kwake.

Mwaka 1995 mwezi wa kumi na mbili(December), kwa mara ya kwanza Miriamu alipata fursa ya kunana uso kwa uso na baba yake mzazi Mzee Lukindo. Miriam anasema pamoja na maongezi yote anakumbuka alimwambia babaye neno moja la msingi kuwa “ Nimefurahi kukujua ”

Miriam akitoa msaada kwenye kituo cha watoto wadogo wenye mtindio wa ubongo jijini Dar es salaam
Baada ya masomo yake ya sekondari Miriamu alipata nafasi ya kundelea na masomo ya chuo katika jiji la Nairobi nchini Kenya. Kwa mujibu wa Miriam akiwa nchini humo ndipo hasa kipaji chake cha uimbaji kiliweza kuchanua vizuri .Akiwa nchini Kenya alikuwa akisali katika kanisa la Maximum Miracle Centre lililo chini ya Mchungaji na muimbaji mahiri nchini humo aitwaye Pastor Pius Muiru.


Chini ya Pastor Muiru Miriam alikuwa kingozi wa sifa na kuabudu kanisani hapo. kanisa hil ndilo mzizi wa kundi Maarufu la muziki wa injili nchini humo liitwalo Maximum Melody. Katika kipindi hicho Miriam anasema alipitia masaibu mengi ya kumkatisha tamaa kimaisha lakini Kristo alikuwa akimtetea na hatimaye alifanikiwa kurekdi album yake ya Kwanza aliyoiita Amen Amen mwaka 2000

Baada ya kurekodi album hiyo nchini Kenya, Miriam aliamua kurudi nyumbani Tanzania. Alipofika Tanzania kwa kuwa Baba yake na Mama yake hawakuwa pamoja na bibi yake akiwa mbeya ilimuwia vigumu namna ya kuweza kuishi katika jiji la Dar es salaam. Kwa bahati rafiki yake mmoja alikubali kuishi naye.  katika kipindi hicho Miriam aliamua kufanya huduma kwa nguvu na Album yake ilkubaliwa vyema na watu mbali mbali hivyo kwa sehemu ikawa Faraja kwa Miriam.
Crew ya Hosanna Inc ikifanya mahojianono na Miriam Lukindo katika Hotel ya Sparrow
Miriam anasema moja kati ya changamoto alizokutana nazo katika huduma yake ni kutunga nyimboo na kujikuta watu wengine wakiingia studio na kuzirekdi. Anasema miaka ya nyuma alitunga nyimbo maarufu iitwayo ya NIGUSE TENA, pamoja na SEMA NA MOYO WANGU na kwa kuwa zilikuwa zake hivyo aliziimba Live mara kwa mara alipokuwa akiitwa kufanya huduma, na kipindi hicho ndipo kundi maarufu la Krystaal lilikuwa nchini Tanzania.

Miriam akiwa na mwanamuziki wa injili Marion Shanko toka nchini kenya
Baada ya muda alizisikia nyimbo hizo zikiwa tayari zimeibwa na kundi hilo lenye makazi yake nchini Uingereza ambapo awali lilikuwa  nchini Canada. Miriam anasema kwanza jamaa walizirekdi kwa Kiwango cha juu mno kuanzia Uwezo wa wa sauti mpaka standard ya muziki wenyewe, hivyo hakuna sababu ya kuwawekea vikwazo. 

Mwaka 2005 krystaal walipokuja Tanzania kwenye mkutano wa Mwakasege ambapo Miriam nayeye alialikwa kuhudumia, Miriam aliwauliza kwa nini mliamua kurekodi  nyimbo hizo pasipo kuniambia, Krystaal wa walimjibu kuwa walijua kuwa hizo ni pambio tu hivyo wakaamua kuzichukua na kuzirekodi serius.

Mwaka 2005 Miriam alifunga ndoa na mhadhili wa chuo kikuu cha Dar es salaam (UD) na Mwanasaikolojia maarufu nchini aitwaye Chriss Mauki. Chriss kwa sasa yuko nchini Afrika ya kusini akisomea shahada ya Uzamivu(Ph.D). Miriam anasema mara baada ya kuolewa aliamua kutulia kidogo pasipo kutoa album ili aweze kujifunza maisha ya ndoa, miaka miwili baadaye yaani Mwaka 2008 akishirikiana na mumewe aliweza kutoa album aliyoipa jina la Ni Ahsubuhi.
Miriam Lukindo akiwa na Mumewe Chriss Mauki
Aliamua kuipa album hiyo jina hilo kwa kuwa aliona kuwa anaanza upya kwa kila kitu katika maisha yake. Hii ni baada ya kupitia mapito mbalimbali hivyo aliona ni kama maisha yameanza upya hivyo ni asubuhi.

Album hiyo hakuifanyia video  mpaka mwaka jana 2010 ambapo alianza kushoot video ya album yake hiyo chini ya kampuni ya Haak Neel Prductin. Miriam kwa sasa yuko chni ya Lebo ya kampuni hiyo, na alifanikiwa kuzindua video ya album hiyo mwaka huu mwezi wa nne katika ukumbi wa Diamnd Jubelee.
Miriam Lukindo akiwa jukwaani wakati wa uzinduzi wa album yake ya Ni Asubuhi katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza
Yafuatayo ni maswali na majibu baina ya Hosanna Inc pamoja na Miriam

H.Inc: Katika labum yako ya Ni Asubuhi kwa nini ulimchagua Jackson Benty kuimba pamoja nawe ilihali Tanzania kuna waimbaji wengi wa kiume?
Miriam: Ni kweli Tanzania kuna waimbaji wengi wazuri lakini nilimchagua Benty kwa kuwa Benty analadha ya Worship, Benty ni worshiper.

H.Inc:Kwa mtu anayekufahamu au kukufuatilia katika huduma yako ya uimbaji, anaweza kukubaliana na Hosanna Inc kuwa Miriam umekuwa ukifanya vizuri sana katika nyimbo za kuabudu(worship) kuliko nyimbo za sifa(Praise), nini hasa kinachopelekea hali  hiyo?
Miriam: Mimi nafanya muziki wowote sifa, pamoja na kuabudu,  ila ni kweli kwenye eneo hilo nimekuwa nikifanya vizuri zaidi kwa kuwa katika huduma yangu Mungu alinitamkia kuwa ”kwenye Worship ndio nitakaa hapo”

H.Inc: Kitu gani kilichopelekea utunge wimbo wa Anasikia?
Miriam: Kuna kipindi nilikuwa nasafiri wakati niko Kenya na sikuwa na pesa ya kutosha hivyo niliomba msaada kwenye yale magari makubwa  ya mizigo, wao waliniambia kama unaweza kaa huko nyuma pamoja na mizigo, nami nikakubali hivyo nikiwa humo ndani ya Lorry ndipo idea ya wimbo huo ikaja kuwa Mungu anasikia.

H.Inc:Tumeshuhudia waimbaji wengi wanakuja na kupotea lakini wewe toka miaka hiyo ya 2000 mpaka leo upo katika huduma hii, nini hasa kinachokufanya ubakie katika ene hili la uimbaji?
Miriam: Kwa kifupi ni lazima ujue  wewe ni nani kwa mantiki ya kujua misingi ya huduma uliyonayo Je umeitwa au umechaguliwa kuifanya huduma hiyo? Mi nina wito na huduma hii ndio maana mpaka leo natumika katika eneo hili.

H.Inc: Kwa nini uliamua kufanya video na Haak Neel Prductin na si kampuni lingine?
Miriam: Kuna makampuni mengi yalinifata ili kufanya nayo video lakini sikuwa radhi kufanya hivyo kwa kuwa kuna kiwango fulani cha ubora nilikuwa nakitaka. Walipotokea Haak Neel niliona ndio wenye uwezo huo kwa kuwa wanavifaa vya kutosha, pia hawana utaratibu wa muda kuwa tunafanya video kwa wiki moja tu na kumaliza, lakini hawa tunafanya na na kurudia kadri tuwezavyo. Hii album ya Ni Asubuhi ina nyimbo nane, na nimeshoot nao kwa miezi tisa sasa  unaweza jionea tofauti.


Hosanna Inc inamtakia kila la heri Miriam na Familia yake katika huduma ambayo Mungu amewaitia.



3 comments:

  1. MUNGU AKUBARIKI SANA MIRIUM, HUWA NABARIKIWA SANA NA NYIMBO ZAKO

    ReplyDelete
  2. Amen good singer Miriam lukindo keep on singing and praising the name of Jesus Christ,On my side I have heard the new albam known as AMEFANYA,THIS ALBAM ESPECIALLY THE SONG CALLED AMEFANYA MADE ME TO BE STRONG IN FAITH THAN I WAS,SO IM SO HAPPY WITH YOUR STORY AND THROUGH THIS STORY I HAVE LEARNT THAT WITHIN IN MY LIFE ICAN FACE DIFFERENT CHALLENGES ,STILL YOU CAN PROCEED DOING WHAT YOU HAVE PLANNED IN YOUR MIND,THANK YOU FOR YOUR MINISTRIES I HOPE ONE DAY YOU WILL BE A GOSPEL SONG TEACHER.
    THANK YOU MY SISTER MIRIAM LUKINDO WA MAUK,
    ELIA SANGA WA IRINGA
    TANZANIA.

    ReplyDelete
  3. Amen good singer Miriam lukindo keep on singing and praising the name of Jesus Christ,On my side I have heard the new albam known as AMEFANYA,THIS ALBAM ESPECIALLY THE SONG CALLED AMEFANYA MADE ME TO BE STRONG IN FAITH THAN I WAS,SO IM SO HAPPY WITH YOUR STORY AND THROUGH THIS STORY I HAVE LEARNT THAT WITHIN IN MY LIFE ICAN FACE DIFFERENT CHALLENGES ,STILL YOU CAN PROCEED DOING WHAT YOU HAVE PLANNED IN YOUR MIND,THANK YOU FOR YOUR MINISTRIES I HOPE ONE DAY YOU WILL BE A GOSPEL SONG TEACHER.
    THANK YOU MY SISTER MIRIAM LUKINDO WA MAUK,
    ELIA SANGA WA IRINGA
    TANZANIA.

    ReplyDelete