Home

Monday, July 11, 2011

Picha Yetu Jumatatu Hii:Askofu Kakobe alipotembelea ofisi za Gazeti la Nyakati

Askofu mkuu wa kanisala Full Gospel Bible Fellowship Askofu Zacharia Kakobe, akikaribishwa katika ofisi za gazeti la Nyakati. Katika ziara hiyo Askofu Kakobe alitoa kiasi cha Shillingi milioni mbili za Kitanzania kwa ajili ya kuikarabati ofisi za gazeti hilo.


Mchango huo ulitolewa kipindi ambapo gazeti hilo mahiri nchini likiwa bado changa. Pamoja naye ni Mhariri mkuu Arnold Victor aliyevalia kitenge, Na meneja matangazo Joseph Mwangomo.


Picha kwa hisani ya Nyakati Hotline

No comments:

Post a Comment