Home

Monday, July 11, 2011

Mkutano wa Askofu Kulola katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza

Askofu Moses Kulola akifanya Maombezi katika viwanja vya Furahisha Jijini Mwanza
Askofu Mkuu wa makanisa ya EAGT askofu Moses Kulola  anamalizia  mkutano wa injili katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza. Katika mkutano huo unaohudhuriwa na maelfu ya watu, askofu kulola pamoja na kuhubiri na kuwaleta kondoo wengi kwa Yesu, siku ya ijumaa ya ilikuwa ni maalumu kwa ajili ya maombezi kwa watu wenye shida mbalimbali.

Toka Mkutano huu umeanza watu wengi wamekuwa wakifunguliwa huku wengine wakiyakabidhi maisha yao kwa Yesu. Pamoja na uzee wa askofu kulola, cha kutia moyo watu wengi bado wanashauku ya kuendelea kumsikiliza kwa nia ya kupata hazina ambayo Mungu ameiweka ndani ya Mtumishi huyu.

Askofu wa kanisa la Eagt kanda ya Ziwa Mch Mahene wa kwanza kushoto akifuatiwa na Askofu wa kanisa hilo jimbo la Mwanza Askofu Lamek Nkuba
Kwa mujibu wa maelezo ya Askofu wa kanisa hilo jimbo la Mwanza Askofu Lameck Nkuba, Askofu kulola baada ya mkutano wa Mwanza , anatarajia kuelekea nchini Burundi kwa ajili ya kufanya mkutano mwingine wa injili. Awali kabla ya Mwanza alikoanza mkutano huo jumapili iliyopita, Askofu kulola wiki mbili ziliyopita alikuwa akifanya mkutano katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wachungaji wa kanisa la Eagt jimbo la Mwanza kutoka kulia ni Mch Sylivester Kilulu wa Eagt Igoma , Mch Daniel Kulola wa Eagt Lumala , Mch George Gecha wa Eagt Ilemela , pamoja na Mch Paul Mkenga 

No comments:

Post a Comment