Home

Wednesday, July 6, 2011

Sababu iliyopelekea Elistoni Angai kumpokea Kristo

Elistoni Angai
Aliyekuwa mwanamuziki maarufu wa muziki wa dansi hapa nchini ajulikanaye kwa jina la Elistoni Angai(Farao), hivi sasa ni mtumishi wa Mungu. Kabla ya kukoka Angai aliwahi kufanya kazi kama mwanamuziki katika bendi ya Diamond Sound,na Mashujaa Band kwa sasa ameunda bendi yake ya injili ijulikanayo kwa jina la “Real Revival Vibration” ambayo tarehe 19-06-2011 walizindua album yao ya muziki wa injili pale Diamond Jubelee.

Eliston Angai ambaye pamoja na kuimba pia hupiga gitaa la solo, alisema alishawishika kukoka mara baada ya mkewe pamja na mtoto wake kuponywa na Bwana Yesu kupitia mchungaji Naaman Shauri wa kanisa la World Might Revival Church  lililpo Benzi Beach jogoo jijini Dar es salaam.

Angai anasema baada ya mkewe kujifungua mtoto waliyempa jina la Julius, mkewe alipata matatizo ya miguu hivyo alikuwa akiumwa na huku mtoto wao hakuwa na hamu ya kula chakula. Katika kipindi hicho ndicho mkewe ajulikanaye kwa jina la Hope mlombo alienda kanisani na kufanyiwa maombi na hatimaye mkewe pamja na mwanaye Yesu akawakaponya magnjwa yao.

Baada ya kushuhudia uponyaji huo, na yeye pia alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya mgongo alienda kwa mchungaji huyo na kuombewa. Baada ya kupona Angai akaamua kumkabidhi Yesu maisha yake(kuokoka), sasa ni zaidi ya mwaka toka aamue kufanya uamuzi huo. Mungu aliyefanya maajabu kwa Angai ataendelea kufanya kwa wengi watu zaidi kwa ajili utukufu wake.


No comments:

Post a Comment