Home

Sunday, July 10, 2011

Shindano la kusaka vipaji la “Sunday Best” kuanza tena july 10


Pichani ni crew ya Sunday Best, kutoka kushoto ni Past or Donnie Mcclurkin, Kirk Franklin Erica toka kundi na Marry Marry, pamoja na mwanadada Kim Burrell.
Lile shindamo mashuhuri la kusaka vipaji vya uimbaji wa Muziki nchini Marekani liitwalo “Sunday Best”, linatarajiwa kuanza tena jumapili hii kwa usaili wa kutafuta washiriki(audition).

Hii ni mara ya nne shindano hili linafanyika na litarushwa kwa masaa mawili katika Television inayopendwa sana na watu weusi nchini humo iitwayo Black Entertaiment Television (BET).

Sunday Best ya itaongozwa na Kirk Franklin kama Mc wa shindano hilo kwa mwaka huu huku majaji wakiwa ni wanamuziki mahiri wa muziki injili nchini humo ambao ni Donnie Mcclurkin, Tina na Erica Campbell toka kundi la Mary Mary, pamoja na Kim Burrell.

Katika usaili huo maelfu ya washiriki toka miji ya Dallas Los Angeles na Atlanta watakuwa wakichuana, mwisho wa siku ni washiriki ishirini tu ambao wataingia kambini mjini Atlanta tayari kwa mchuano.

Hosanna Inc itakuwa ikikuletea yanayojiri katika mashindano hayo kwa lengo la kujifunza nini wenzetu wanafanya kwa kuwa hap nchini Gospel star Searches nyingi zimekufa baada ya kumalizika kwa msimu mmoja.

Source:Christian Posts

No comments:

Post a Comment