Home

Monday, August 15, 2011

Classic Gospel Concert Happened in Mwanza

Haihitaji utumie TESTA ili kuweza kujua kuwa Mungu anaitembelea Tanzania na kuweka mwamko wa Tofauti hususani kwenye eneo la Kusifu na kuabudu. Jana 14/08/2011 katika ukumbi wa Nyumbani Hotel jijini Mwanza kulifanyika Tamasha la Kusifu na kuabudu lililoandaliwa na Kanisa la Mwanza International Community Church (MICC) lililo chini ya Pastor Zakayo Nzogelle.

Kuna matamasha mengi yanafanyika lakini hili Mungu alijidhihirisha kwa namna ya tofauti na kugusa mioyo ya Wengi. Hakukua na na Intertaiment na kwa mara ya kwanza kumeshuhudia watu wakisimama kwa muda mwingi wa concert wakimwabudu Mungu na sio kukaa na kuwashangaa waimbaji walioko Madhabahuni.

Taratibu tunahama katika level za kushabikia Burudani za Injili tunaenda kwenye level za kuabudu ambazo zinaugusa moyo wa Mungu. Na kwa wanaofatilia watagundua kwa sasa nchi nzima Matamasha yanafanyika. Arusha wako HOT, Mwanza, Mbeya, Morogoro Dar ndio usiseme hapo utaona pamoja na mapungufu yaliyopo taratibu uchaji halisi unaiteka nchi. 


Concert zinafanyika na watu wengi wanahudhuria pasipo uwepo wa Rose Mhando, Shusho, Nkone wala Prominent figure yeyote. Na hii sio kwa Corncerts tu bali hata makanisani uchaji wa Mungu kupitia sifa na kuabudu unazidi  kuimarika siku hadi siku.

Kuna wengi wanasema Kanisa la Tanzania limejaa migogoro baina ya kanisa na kanisa, watumishi kwa watumishi, watumishi na waimbaji wameweka maslahi yao binafsi  mbele kuliko Ufalme wa Mungu mi nasema FINE wakiri wanavyokiri ila nikionacho mimi ni kuwa Mungu yuko Karakana{Workshop} akjiandalia jeshi lake kwa utukufu wake ambalo kamwe halitopiga MAGOTI kwa Baali.

MICC Praise Team wakiwa wakisubiri zamu yao ifike wapande stejini
Hosanna Praise Team wakiimba

Bro Ado Nzwalla akiongoza sifa katika kikundi cha Hosanna Praise Team

Micc Praise Team wakiwa Jukwaani

Twakupa sifa eeh Bwanaa Milelee milelee milelee Debora Meshak akilead hiyo nyimbo

Pastor Zakayo Nzogelle akiimba pamoja na MICC Praise Team

Dr Nora akilead Praise

Bro Rapha akilead Praise

Umati wa watu ukumbini hapo

Mch Zakayo Nzogelle akiwa na Familia yake baada ya tamasha kumalizika




No comments:

Post a Comment