Home

Monday, August 8, 2011

JIFUNZE KULINDA NA KULISIMAMIA WAZO LA MUNGU NDANI YAKO (Part 2)



Huu ni muendelezo kutoka Somo la jumatatu wiki iliyopita lenye kichwa cha habari  JIFUNZE KULINDA NA KULISIMAMIA WAZO LA MUNGU NDANI YAKO (Part 1) Kutoka kwa Mwl Sanga.

Namna ya kutoka kwenye tatizo ambalo uliingia kupitia maamuzi uliyoyatekeleza. Kumbuka kwenye sehemu ya kwanza ya somo hili niliandika kwamba; Maisha (future) ya mtu ni matokeo ya mawazo jumlisha maamuzi anayotekeleza kwenye maisha yake. Mawazo na maamuzi yako yataamua kile utakachozaa/kitakachofunuliwa, Utakachozaa kitaamua future yako na future yako itaamua mwisho (destiny) yako. 
 

Ukiamua vibaya maana yake umechagua mauti na laana kwenye maisha na future yako. Na hii ina maana mawazo na maamuzi uliyoyatekeleza yanakuweka kwenye eneo la uharibifu/mauti/laana/ na yanakufanya uonekana hufai/useless (Isaya 42:22). Sasa katika sehemu hii ya pili nitafundisha namna ya kutoka kwenye eneo hili la uharibifu ambalo umeingia kwa sababu ya mawazo na maamuzi uliyoyatekeleza;

1. Lazima ulikubali/ukiri tatizo/changamoto na kisha udhamirie kutoka .                                                                              
Ukisoma ile Isaya 50:21 utaona kwamba licha ya mwanandamu kufanya maamuzi mabaya Mungu alinyamaza. Sasa kitendo cha Mungu kunyamaza kwake kunamfanya huyu mtu aone hakuna tatizo. (Zaburi 50:21). Kwa hiyo hatua ya kwanza ni kulikubali tatizo na kisha usiridhike na hali uliyo nayo (tatizo). Kutokuridhika kuendelea kuwepo kwenye hali hiyo kutatengeneza fikra za kutaka kutoka kwenye hilo tatizo kwa mfano natokaje, napitia wapi, naanzaje,nk.

2.Unahitaji kujua wazo na maamuzi yaliyokufikisha mahali ulipo.                                                                                                      Mpaka ukafika mahali ulipo ina maana kuna uamuzi ambao uliutekeleza ulikufanya ukafika hapo. Kwa hiyo fuatilia kujua ni chazno cha uamuzi huo na uamuzi huo ni upi, hii itakusaidia usirudie kutekeleza wazo la awali. Kiroho hii dhana ina maana tafuta ni wapi ulianguka? Rejea kitabu cha (Ufunuo 2:5).

3. Tafuta wazo jipya la kukutoa hapo ulipo (Isaya  48:6).                                                                                                                    
Ukishajua wazo na uamuzi uliokufikisha ulipo tafuta wazo jipya/jingine maana hilo litakupa uamuzi mpya/mwingine. Na mahali pa kuanzia ni Yeremia 29:11 ambayo inatueleza kwamba siku zote mawazo ya Mungu kwetu ni mawazo ya amani/kutufanikisha (positive ideas/thougts of prosperity). Ili kupata mawazo mapya unapaswa kuongeza utajiri kwa ufahamu neno la Mungu ndani yako Wakolosai 2:2 inasema “… Wakapate utajiri wote kwa kufahamu….

4.Ongeza ufahamu wako ili uweze kufanya “informed decisions” .                                                                                                          Siku zote Kiwango cha kuwaza/kuamua kwa mtu kinategemea kiwango cha ufahamu wake. Hivyo ili kufanya maamuzi yaliyo bora taarifa/ufahamu wa kutosha juu ya kile unachotaka kuamua ni kitu cha lazima. Hata watafiti wanasema “No research no right to speak” wakimaanisha kama hujafanya utafiti juu ya kitu Fulani huna haki ya kuzungumza juu ya hicho kitu. Hivyo hakikisha “… Kwa mapato yako yote jipatie ufahamu” (Mithali 4:7) na pia imeandikwa “ asomaye na afahamu”.

5. Jifunze kuitia nguvu/moyo nafsi yako kwa kuisemesha (Zaburi 42:5).               
Katika sehemu ya kwanza niliandika kwamba mtu anapofanya uamuzi mbaya kwenye maisha yake anasabbisha ugonjwa kwenye nafsi yake ambayo ni kiti chake cha hisia. Mtu huyu anasababisha nafsi yake kuinama na hii ina maana hisia zake na kumbukumbu zake zitamjia na kumpa taarifa kwamba wewe ni wa kushindwa tu/huwezi kufanikiwa/hakuna tumaini tumaini mbele yako/maisha yako yatakuwa hivihivi nk.

Sasa ili kutoka hapa unatakiwa kutafuta mistari kwenye Biblia ambayo inalenga kuleta tumaini, furaha, amani, kufanikiwa kwenye nafsi yako. Ifuatayo ni baadhi ya mistari ambayo nimeona ni vema nikuwekee kama dondoo za msingi kwanza, lakini tafuta kwa nafasi yako mistari mingine kwenye Biblia (Make sure u do that). Iambie nafsi yangu usiiname, na kama ikikuuliza kwa nini? Ijibu ukisema;

• Even if now I’m useleess, it is written “the useless becomes useful” (Filemoni 1:11) na hata kama niliingia kihalali kwenye tatizo hili ameahidi kunitoa (Isaya 49:24-26). Maana imeandikwa ‘mimi ni Mungu niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu’ (Isaya 43:25) na ijapokuwa sasa ni giza alifajiri inakuja (Ayubu 11:17)

 • Iambie nafsi yangu, uwe na Positive view of problems. Hii ina maana iambie nafsi yako isilitazame tatitzo kama kikwazo bali ilitazame tatizo kama sehemu ya njia kufikia mafanikio yake. 2 Wakorinto 4:17–18 ‘Tusiviangalie vinavyoonekana maana ni vya muda tu…’ i.e Ugonjwa huu si ugonjwa wa mauti, i.e sitakufa bali nitaishi.

• Ikiwa Mungu aliona kila kitu alichokifanya ni kizuri wewe usijione kwamba ni mbaya. Hebu soma hii mistari kuhusu mtazamo wa Mungu juu ya kazi yake, Mwanzo 1:4, 10, 12, 18, 21, 25, 31. Jifunze kujiona wewe ni mzuri/una pesa/utaolewa/utafanikiwa tu n,k.

• Iambie nafsi yangu hata kama nje nimesikia habari za kunivunja moyo, sitaacha kwenda ibadani, sitaacha kusoma masomo kwenye blog na hata Biblia na hii ni wa sababu imeandikwa “Kwa Bwana zipo habari njema za kuninenepesha mifupa” ( Mithali 15:30) na zaidi “Ahadi zote katika yeye Mungu ni ndiyo na amin” (2 Wakorinto1:18-21)

Tamati; Mpenzi msomaji imeandikwa watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa Ujumbe huu umelenga kukupa maarifa kwa ajili ya maisha yako ya kesho yaani wakati ujao ‘future’ yako kuwa bora. Usikubali kuharibu future na destiny yako. Na ni jukumu lako kuamua aina ya maisha unayotaka kuishi .
“Mungu hana namna ya kumsaidia mtu kama hataweza kulitii neno lake” narudia tena “Mungu hana namna ya kumsaidia mtu kama hataweza kulitii neno lake” Asomaye na afahamu.
Ubarikiwe na Bwana Yesu na tuzidi kuombeana

Mwl Sanga

2 comments: