Home

Saturday, August 6, 2011

Mtumishi Daniel Kulola Kufanya Huduma jijini Nairobi na Denmark


Mch Daniel Kulola na Mkewe
Mtumishi wa Mungu Pastor  Daniel Kulola anatarajia kuondoka nchini Tanzania  kesho tarehe 7/08/2011 kwenda jijini Nairobi kwa ajili ya kuhudumu katika Kongamano la Kimataifa liitwalo “Burning Fire” linalotarajia kuanza jumatatu ijayo na kumalizika Jumapili aijayo.

Kongamano hilo lililoandaliwa na Pastor Ken Kamau wa kanisa la Gospel Revival Centre – Kawangware litahudhuriwa pia na watu kutoka mataifa mbalimbali ambayo ni South Africa, America, Ufaransa, kenya, Malawi na Zambia. Pastor D. Kulola  ameiambia Hosanna Inc kuwa katika kongamano hilo atahudumu siku ya jumatatu na jumanne ambapo kwaya ya  Uinjilisti – Lumala kutoka kanisani kwake EAGT Lumala Mwanza itakuwa ikihudumu pia katika Kusanyiko hilo.

Siku ya Jumatano Mch Kulola atakuwa akirudi Mwanza kwa ajili ya Maandalizi ya Safari ya kitumishi kuelekea Denmark . Tar 16 August 2011 Mch kulola pamoja na mkewe watakuwa wakielekea kufanya huduma nchini Denmark katika jiji la Copenhagen chini ya kanisa la “The Narrow Gate church” mkutano ambao umeunganisha makanisa mbalimbali ya jiji hilo.

Kwa yeyote atayependa kumsapoti Mtumishi Daniel Kulola kwa maombi ili kufanikisha utumishi huu anaombwa afanye hivyo. Na kwa wale wanaopenda kumsapoti kwa fedha usisite tumia njia zifuatazo.
CRDB MWANZA Daniel Moses Kulola
01j2053306700

Kenya commercial Bank Daniel&Mercy Kulola 
018100004710

MPESA 0767749040.

Mbarikiwe na Bwana Yesu.

No comments:

Post a Comment