Home

Saturday, August 6, 2011

Friends on Friday II Yawagusa Wengi


Ule usiku uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na watu mbalimbali jijini Dar es salaam na nje ya jiji hilo ujulikanao kama Friends on Friday ulifanyika usiku wa jana na kuwabariki wengi waliohudhuria. Friends On {FoF}  ni usiku ambao huwakutanisha watu mbalimbali waliokoka  kila ijumaa ya mwisho wa mwezi au mwanzo wa mwezi na kukaa pamoja kubadilishana ideas na kufurahi.

Katika FoF ya jana iliyofanyika katika Hotel ya Tamal iliyopo Mwenge jijini Dar es salaam ilihudhuriwa na watumishi wa Mungu mbalimbali wakiwemo waimbaji maarufu wa injili nchini Tanzania kama John Lissu, Jackson Benty, Flora Mbasha, Glorious Band, Calvary Band, Bro Hondo wa New Life Band pamoja na wengine wengi.

Hii ni FoF ya pili kufanyika baada ya ile iliyofanyika mwezi wa sita mwaka huu, FoF II iliyopewa jina la “FoF Amplifier”  ilihudhuriwa na zaidi ya watu mia mbili ambapo awali walioweza kukonferm kwa kununua tiketi kabla ya ijumaa walikuwa 170 ila siku ya tukio yaani jana waliongezeka watu zaidi ya thelathini kitu ambacho ni changamoto kubwa kwa Timu nzima iliyoandaa Event hiyo.

Paul Mashauri mjasiliamari maarufu nchini aliweza kutoa darasa la ujasiliamali kwa waliohudhuria huku Calvary Band ilikuwepo na kupiga LIVE.

Wadau wakiwa ukumbini hapo njano ndio ilikuwa Rangi  ya Event hiyo

Hii combination ya njanio na Nyeusi ilitengeneza kitu cha ukweli
Mbarikiwa Sanga Lecturer wa Saint John University alifika akitokea Dodoma kuhudhuria Event Hiyo


Tumbo ni Kwa Chakula na Chakula ni kwa Tumbo

Charting zikiendelea

Hahaaaaaaa  Mc Luvanda na mshkaki

Miriam Lukindo na Flora Mbasha wakiimba kwa pamoja ukumbini Hapo

Watu walijumuika kucheza ukumbini hapo

Watumishi wakienda sawa na Bendi ya Calvary


Hii ndiyo Kamati ya Maandalizi ya FoF II

No comments:

Post a Comment