Home

Sunday, November 20, 2011

Sunday Sermon:Karama za Roho Mtakatifu 2



2) Karama ya imani na matendo ya miujiza:

Karama ya imani na ya matendo ya miujiza ni kama zinafanana. Katika hizi mbili, mwenye kutumiwa hupokea ghafula imani kwa ajili ya yasiyowezekana. Tofauti kati ya hizo mbili mara nyingi hufafanuliwa kama ifuatavyo: Kuhusu karama ya imani, ni kwamba yule anayetiwa upako hupewa imani ili apokee muujiza kwa ajili yake mwenyewe, ila, kwa habari ya karama ya matendo ya miujiza ni kwamba, mhusika hupewa imani ili kutenda muujia kwa ajili ya mwingine. 

Karama ya imani wakati mwingine huitwa “imani maalum” au ya kipekee kwa sababu ni kupewa imani inayozidi ya kawaida. Imani ya kawaida huja kwa kusikia ahadi ya Mungu, wakati ambapo imani maalum huja kwa toleo la ghafula la Roho Mtaka tifu. Wale ambao wamewahi kufahamu karama hii ya imani maalum hutaarifu kwamba mambo ambayo walikuwa wanayahesabu hayawezekani yanawezekana, na ukweli ni kwamba wanajikuta haiwezekani kuwa na shaka. Mambo ni hivyo hivyo kuhusu karama ya matendo ya miujiza.
Habari ya rafiki watatu wa Danieli – Shadraka, Meshaki na Abednego – ni mfano mzuri sana jinsi ambavyo “imani maalum” inavyofanya isiwezekane kuwa na shaka.


Wakati walipotupwa katika tanuru la moto kwa kukataa kusujudia sanamu ya mfalme, wote walipewa karama hiyo ya imani maalum. Kweli – kukubali kuingia katika tanuru la moto mkali kulihitaji imani zaidi ya kawaida! Hebu tutazame imani waliyo-onyesha hao vijana watatu, mbele ya mfalme.

Ndipo Shadraka na Meshaki na Abednego wakajibu, wakamwambia mfalme, Ee Nebukadreza! Hamna haja kukujibu kat ika neno hili. Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto; naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme. Bali kama si hivyo [yaani, kama hutatutupa katika tanuru hiyo ya moto], ujue ee mfalme ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hio sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha (Danieli 3:16-18. Maneno mepesi kukazia).

Ona kwamba karama ilikuwa inafanya kazi hata kabla hawajatupwa katika tanuru la moto. Hapakuwa na shaka katika akili zao kwamba Mungu angewakomboa.
Eliya alifanya kazi chini ya karama hiyo ya imani maalum wakati alipolishwa kila siku na kunguru, katika kipindi cha njaa ya miaka mitatu wakati wa utawala wa Mfalme mwovu, Ahabu (ona 2Waf. 17:1-6). Unahitaji imani ya ziada kumwamini Mungu kwamba atatumia ndege wakuletee chakula asubuhi na jioni. Ingawa Mungu hajatuahidi popote katika Neno Lake kwamba kunguru watatuletea chakula kila siku, tunaweza kutumia imani ya kawaida kumtegemea Mungu kwamba mahitaji yetu yatatoshelezwa – kwa sababu hiyo ni ahadi iliyopo (ona Mat hayo 6:25-34).

Matendo ya miujiza yalifanyika mara kwa mara katika huduma ya Musa. Karama hii ilikuwa kazini wakati alipogawa Bahari ya Shamu (ona Kutoka 14:13-31), na mapigo mbalimbali yalipoishukia nchi ya Misri.

Karama hii ilikuwepo katika huduma ya Yesu wakati alipowalisha watu elfu tano kwa kuongeza mikate michache na samaki (ona Mathayo 14:15-21).
Mfano mwingine wa karama hii ni wakati Paulo alipomfanya Elima mchawi kuwa kipofu kwa muda kwa sababu alikuwa anapingana na huduma yake pale kisiwani Kipro (ona Matendo 13:4-12).

Karama Za Ufunuo

3) Neno la maarifa na neno la hekima:
Karama ya neno la maarifa mara nyingi hufafanuliwa kwamba ni kupewa kwa ghafula kufahamu habari fulani, ya wakati uliopita au uliopo. Mungu ambaye ana maarifa yote, wakati mwingine atatoa kiasi kidogo cha maarifa hayo. Pengine ndiyo sababu huitwa neno la maarifa. Neno ni sehemu ndogo ya sentensi, na neno la maarifa linaweza kuwa sehemu ndogo ya maarifa ya Mungu.

Neno la hekima ni sawa tu na neno la maarifa, ila mara nyingi hufafanuliwa kama uwezo wa ghafula usio wa kawaida, wa kujua matukio yajayo. Wazo la hekima mara nyingi huhusiana na kitu fulani cha baadaye. Hapa tena si kwamba tafsiri hizi ni kamilifu.
Hebu tutazame mfano wa Agano la Kale kuhusu neno la maarifa. Baada ya Elisha kumtakasa ukoma Naamani Mshami, Naamani alimpa Elisha fedha nyingi sana kama shukrani kwa kuponywa. 


Elisha alikataa zawadi hiyo, mtu yeyote asije akafkiri kwamba uponyaji wa Naamani ulinunuliwa badala ya kutolewa na Mungu kwa neema tu. Mtumishi wa Elisha aliyeitwa Gehazi, akaona nafasi ya kujipatia utajiri binafsi, naye kwa siri akapokea kiasi fulani cha malipo yaliyokusudiwa kumfikia Naamani. Baada ya Gehazi kuficha fedha yake aliyopata kwa udanganyifu, alisimama mbele ya Elisha.

Tunasoma hivi:Elisha akamwambia, Watoka wapi Gehazi? Akanena, Mtumwa wako hakuenda mahali. Akamwambia, Je! Moyo wangu haukwenda na wewe, hapo alipogeuka yule mtu katika gari ili akulaki? (2Waf. 5:25b, 26a).
Mungu ambaye alifahamu vizuri tendo baya la Gehazi, alimfunulia nabii Elisha kwa njia ya ajabu. Habari hii inaonyesha dhahiri ya kwamba Elisha “hakumiliki” karama ya neno la maarifa – yaani, hakujua kila kitu kuhusu kila mtu kila wakati. Kama ingekuwa hivyo, Gehazi asingeota ndoto kwamba angeweza kuficha dhambi yake.

Elisha alifahamu vitu kwa njia isiyo ya kawaida wakati tu Mungu alipomfunulia vitu hivyo, mara kwa mara. Karama ilifanya kazi kama Roho alivyopenda.
Yesu alitumia karama hiyo wakati alipomwambia yule mwanamke pale kisimani Samaria kwamba alikuwa na wanaume watano (ona Yohana 4:17, 18).
Petro alitumia karama hii wakati alipojua kimuujiza kwamba Anania na Safira walikuwa wanadanganya kusanyiko kwamba walichokuwa wanatoa ndiyo bei kamili ya uwanja wao waliokuwa wameuuza karibuni (ona Matendo 5:1-11).

Kuhusiana na karama ya neno la hekima, inadhihirishwa mara kwa mara katika Agano la Kale kwa manabii wote. Kila walipotabiri tukio la wakati ujao, neno la hekima lilikuwa kazini. Yesu alipewa karama hii mara kwa mara pia. Alitabiri kuhusu kuharibiwa kwa mji wa Yerusalemu, kuhusu kusulubiwa Kwake, na matukio ambayo yangetokea duniani kabla ya kuja Kwake mara ya pili (ona Luka 17:22-36; 21:6-28).

Mtume Yohana alitumiwa katika karama hii wakati alipofunuliwa zile hukumu za Wakati wa Dhiki Kuu. Ametuandikia hayo yote katika Kitabu cha Ufunuo.

Heaven Family

No comments:

Post a Comment