Home

Thursday, March 8, 2012

Baadhi ya wanawake Mashuhuri wanaomtangaza Kristo Nchini



Leo tarehe 8/03/2012 ni siku maalumu ya wanawake duniani, kwenye Biblia kuna orodha ndefu ya wanawake waliosimamia makusudi ya Mungu katika Mazingira na vipindi tofauti tofauti.Biblia inaonyesha wazi namna ambavyo kina Debora, Abigaili, Dorcas, Esta na wengine wengi.Hapa nchini wapo wanawake WENGI wanaoutangaza Ufalme wa Mungu kwa utukufu wa Mungu.Baadhi ya wanawake ni kama ifuatavyo

Mama Catherine Abihudi

Mch Catherine Abihudi
Mch Catherine Abihuni ni mtumishi wa Mungu ambaye kwa sasa anamtumikia Mungu akiwa nchini Marekani pamoja na Mumewe Mch Charles  Abihudi.Kabla ya kwenda marekani alikuwa ni mmoja kati ya wanawake waliogusa mioyo ya watu wengi nchini kwa ujasili wake na uwezo wa kufundisha Neno la Mungu with revelations.

Amekuwa akisaidia sana Vijana wa vyuoni na Makanisani na kwa sasa akishirikiana na watumishi wengine huandaa Makongamano ya Pasaka nchini Marekani.Kabla ya kwenda Marekani yeye na mumewe  walikuwa wakihudumu katika kanisa la Calvary Asemblies of GOD lililoko chini ya Apostle Danstan Maboya

Alice Prosper Ntepa Mtoto wa Mama Prosper Ntepa
 .
Mama Prosper Ntepa
Mama Mchungaji na mke wa mtumimishi wa Mungu Prosper Ntepa,mama Ntepa kwa muda mrefu sasa amekuwa mchungaji na ameandaa semina nyingi za kimungu zenye lengo la kumbomboa mwanamke.Tofauti na kuhubiri madhabahuni Mama Ntepa anaaminika ndiye Mtumishi wa Kwanza mwanamke nchini kuandika vitabu vingi vinavyohusiana na maisha ya ukristo.


Mama Kimaro

Mama Kimaro wa Mwanza
Mch Mama Kimaro wa huduma ya Divine Favour iliyoko Nyakato jijini Mwanza, ni mmoja kati ya wamama walioamua kuingia kwenye huduma.Kabla ya kuanzisha Divine Favour Mama Kimaro alikuwa Mchungaji chini ya Huduma ya Cathedraw of Joy inayoongozwa na Askofu John Komanya.

Mch Getrude Rwakatare

Mama Getrude Rwakatare
Mama Getrude Rwakatare ni Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Mikocheni B Asemblies of GOD(Mlima wa Moto).Pamoja na kufanya mengi nchini, Mama Rwakatare amechunga kanisa kwa muda mrefu sasa na amekuwa ni Mchungaji wa Kwanza Mwanamke kuingia Bungeni kama Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mama Diana Mwakasege

Mama Diana Mwakasege
Ni wazi kuwa kukua na kufanikiwa kwa huduma ya Mwl Christopher Mwakasege kwa kiasi kikubwa kumetokana na Ufanisi na jitihada za ubavu wake mama Diana Mwakasege.Amekuwa mstari wa mbele kuwaleta watu kwa YESU, kufundisha semina za Vijana na Ujana  pamoja na kuwaombea Roho mtakatifu wale wote wenye kiu ya kujazwa Roho wa MUNGU na MUNGU amekuwa akionekana katika Maombezi hayo.

Dada Mary Damian

Mary Damian
Mtumishi Mary Damian huyu ni binti na mmiliki wa Blog ya kwanza maarufu nchini iitwayo STRICTLY GOSPEL. Miaka kadhaa iliyopita alianzisha blog hiyo ambayo imewagusa wengi nchini kwa mijadala na uchambuzi wa kina wa Neno la Mungu pasipo kujali udhehebu.Kwa sasa  Mary yuko Masomoni nchini Marekani.

Mama Mchungaji Debora Kaisi

Mama Debora Kaisi
Kwa watu wanye historia ya kutosha kuhusu Manzese uwanja wa fisi watakuwa wanajua nini kilikuwa kinafanyika katika viwanja hivyo, palikuwa ni mahali ambapo starehe za kila aina with cheap Price zilikuwa zikifanyika kwa viwango vya juu.Unywaji wa pombe zote za kienyeji pamoja na biashara ya ukahaba vilikuwa vimeweka kambi mahali hapo. Mch Debora Kaisi na mumewe waliliona hilo na hivyo kuingia kazini kwa kumsihi Roho wa Mungu alibadilishe eneo hilo.

Mama Kaisi na mumewe kwa sasa wamefungua kanisa mahali hapo na watu wanamuabudu Mungu na kwa hili Hosanna Inc tunasema ni EBENEZER.Kwa sasa hapaitwi tena uwanja wa Fisi bali panaitwa UWANJA WA SIFA.Tofauti na hayo amekuwa akiendesha semina mbalimbali za mabinti na wanawake kanisani kwake na katika makanisa mbalimbali.

Dada Rose mushi

Rose Mushi
Dada Rose mushi ni mtumishi wa mungu kijana ambaye amebadilisha fahamu za watu wengi kwa kutumia vitabu.Mpaka sasa ameandika vitabu takribani vitano vinavyoelezea general things kwenye jamii kwa mlengo wa bIblia.Vijana wengi nchini wana-potential nyingi ila hawataki ku-dig deep into their potentials na mwisho wa siku hizo precious potentials zinapotea.Dada Rose Mushi ameliona hilo na vitabu vyake vimekuwa baraka kwa wengi na kwa kanisa kwa ujumla.

Mama Lilian Ndegi

Mch Lilian Ndegi
Mama Lilian Ndegi ni mke wa Apostle Onesmo Ndegi wa huduma ya Living Water Kawe Makuti. Kwa muda mrefu sasa amekuwa akiendesha semina za neno la Mungu zinazohusu Wanawake kwa ushirikiani mkubwa wa watumishi wengine.Amekuwa bega kwa bega katika kuaendesha semina hizo kwa ushirikiano wa Mama Ntepa,na mama Debora Kaisi Pamoja na wengine wengi.




Mama Tedy Kwilasa
Ni vigumu sana kumsahau huyu Mama,Mama kwilasa anaongoza huduma ya Victory Ministry yenye makao yake makuu jijini Dar es salaam. Kwenye marketing kuna neno la Kimaketia linaitwa “Marketing Segmentation” na Kimungu kuna kitu kinaitwa “Centre of the Vision”.Mama kwilasa kwa sehemu kubwa amebase(segment/centre of her vision ni) kwa wadada.Amekuwa akiendesha semina nyingi za wadada katika vyuo mbalimbali na ni Mmoja kati ya Wamama wanaohubiri katika Mikutano ya Nje.


No comments:

Post a Comment