Home

Sunday, March 11, 2012

Kwa Heri FOI wa Maximum Melodies

Andrew Young kushoto with wireless Microphone akiwaongoza Maximum Melodies kwenye Mazishi hayo
 Ijumaa iliyopita ya Tarehe 9/03/2012 yalikuwa ni Mazishi ya Mtumishi wa Mungu Winifrida Wambua maarufu kwa jina La FOI,katika uhai wake FOI alikuwa member wa kundi la Muziki wa Injili liitwalo Maximum Melodies la jijini Nairobi.Alikuwa ni solo wa kundi hilo na aliwabariki wengi kwa utumishi wake.

Ijumaa ya tarehe 02/03/2012 FOI alifariki kwa ajali alipokwa akienda kuhudhuria moja ya vikao vya kundi hilo na ndipo alipogongwa na lori katika moja ya mitaa ya jiji la Nairobi.Katika Mazishi hayo yaliyohudhuriwa na watu wengi,Kundi la Maximum Melodies chini ya kiongozi wa kundi hilo Andrew Young walipata nafasi ya Kuimba kama ishara ya kumuaga Mwenzao.

Maximum Melodies wakumuaga FOI.

Kwa Heri FOI

No comments:

Post a Comment