Home

Sunday, March 11, 2012

Sunday Sermon:Utendaji Kazi Wa Karama Za Roho

Mwl Christopher Mwakasege
I Wakorintho 14:12; ''Vivyo hivyo na ninyi kwa kuwa mnatamani sana kuwa watu wenye karama za roho, takeni kwamba mzidi sana kuwa nazo ili kulijenga kanisa''.
UTENDAJI KAZI WA KARAMA.

Mambo muhimu (ya msingi) kufahamu ili karama za Roho Mtakatifu ziweze kufanya kazi. Mambo hayo ni

1.) kubali kuwa karama za Roho zinaweza kufanya kazi kwako pia. I Wakorintho 12:4.11; ''Basi pana tofauti za karama bali Roho ni yeye yule, lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye''. Roho Mtakatifu ndani ya mtu anazo karama zote bali anamgawia kila mtu kama apendavyo yeye. Rumi 12:3-6; inasema ''kwa maana kwa neema niliyopewa na mwambia kila mtu aliyeko kwenu asinie makuu kupita ilivyo mpasa kunia ..........., basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali.

2.) Uwe na hamu (haja) kubwa ya msaada wa Mungu. I Wakorintho:1,12; ''ufuateni upendo na kutaka sana karama za rohoni, lakini zaidi kwamba mpate kuhutubu, vivyo hivyo na ninyi kwa kuwa mnatamani sana kuwa watu wenye karama za roho, takeni kwamba mzidi sana kuwa nazo ili kulijenga kanisa''.
Angalizo: karama siku zote zina mvuto.

3.) Tembea katika wito (nafasi) yako. Warumi 12:6, ''......... kwa kadri ya neema tuliyopewa...'', yaani wito (kiwango) ulichopewa. Ndani ya wito kuwa nafasi ambayo Mungu amekupa. Kuna ngazi, kuna mahali na muda unaotakiwa kuufanyia huo wito. Galatia 2:6-7 ''......walipokwisha kujua neema niliyopewa........ walinipa mimi mkono wa kuume wa shirika''.
Mfano: kuna tofauti ya karama ya unabii na huduma ya unabii, yaani kila mtu aliyeokoka anaweza kutoa unabii bali si kila mtu ana karama ya unabii.

4.) karama kutenda kazi vizuri ndani ya mtu inategemea kiwango cha Imani alichonacho. Rumi 12:6; ''basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali ........ ikiwa unabii tutoe unabii kwa kadri ya imani''. Sio zaidi ya hapo. Rumi 10:17; ''imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa neno la kristo'' yaani kiwango cha imani ulichonacho hakiwezi kuzidi hapo. Imani huja tu kwa neno la Kristo. Biblia haituruhusu kutembea kwenye karama zaidi ya imani tuliyo nayo.
 
Angalizo: kufahamu neno la Kristo kwa wingi ni muhimu. Tembea katika karama za roho kwa kadri ya imani.


No comments:

Post a Comment