Home

Tuesday, July 31, 2012

Love Tanzania Festival kuyakutanisha zaidi ya Makanisa 800 nchini



Miwani 10,000 za kusomea kugawiwa Bure
Wafanyabiashara wakubwa na viongozi wa serikari kuinjilishwa kupitia Evening Dinner
Kikundi maalumu cha Michezo ya Baiskeli kuonyesha ufundi wa kuchezea baiskeli
Tofauti na Donnie Moen, Nicole C Mullen  ,Christina  Shusho,John Lissu,Pastor Safari Paul wa DPC kuongoza Love Tanzania Festival Praise Team

Love Tanzania Festival ni kusanyiko kubwa la kihistoria litakalofanyika kuanzia tarehe 11-12/08/2012 katika viwanja vya Jangwani kuanzia saa saba mchana mpaka saa 2 Usiku.Kwa mujibu wa mmoja wa waandaaji wa kusanyiko hilo Brother Prosper Mwakitalima ameiambia Hosanna Inc kuwa katika kufanikisha kusanyiko hilo makanisa zaidi ya 800 yameshiriki katika maandalizi ya tukio hilo maalumu lenye lengo la kuwakutanisha watu wa dini,kabila,rika zote kwa lengo la kumtukuza Kristo Yesu.

Kwa mujibu wa Mwakitalima kabla ya shughuli ya tarehe 11 na 12 kuna shughuli mbalimbali ambazo Love Tanzania Festival itakuwa ikizifanya kwa jamii ya Tanzania.

Ifuatayo ni Ratiba ya shughuli nzima za LOVE TANZANIA FESTIVAL.

Tarehe 5 August  7:00Asbh – 10.00 Asbh
Mbeba maono wa Love Tanzania Featival  mtumishi Andrew Palau atahubiri ibada zote mbili katika kanisa la Upanga City Christian Centre (UCC)

Muimbaji mashuhuri Nicole C Mullen atahudumu

Tarehe 7 August 10Asbh
Kutafanyika Mkutano wa waandishi wa habari(Press Confference) katika Ukumbi wa TBD ambapo Andrew Palau akiambatana na wachungaji, Maaskofu,waimbaji na kikundi cha waonyesha michezo ya Baiskeli watakuwa wakiongea na waandishi wa habari.
Usiku huo wa Tarehe 7 kuanzia saa 11.30 jioni katika ukumbi wa KARIMJEE  kutafanyika WOMENS DINNER ambapo kamati imewakaribisha zaidi ya wamama 600 nao watapata nafasi kusikiliza na ya kubadilishana mawazo na Andrew Palau.

Tarehe 8 August  12:00 jioni
Katika Ukumbi wa Karimjee Hall kutafanyika hafla ya chakula cha jioni ambapo viongozi mbalimbali wa serikali na wafanyabiashara wakubwa watapata nafasi ya kukutana na Palau ambapo mtumishi huyo atatumia nafasi hiyo kumtangaza kristo kwa tabaka hilo la watanzania ambao kwa namna moja au nyingine limekuwa ni vigumu kufikiwa na injili ya Yesu kristo.

Tarehe 10:August 8:00 Mchana – 9:00 Jioni
Kutafanyika maozoezi(Rehesal)ya michezo ya Baiskeli ambapo kikundi cha JUNGLE RUSH FMX  kutoka Afrika ya Kusini kitakuwa kikifanya mazoezi hayo ili kujiweka sawa.Baada ya mazoezi hayo kutafanyika MAOMBI rasmi kwa ajili ya kuuweka wakfu uwanja wa Jangwani kwa ajili ya shughuli nzima ya tarehe 11-12.



VITUO MAALUMU KWA AJILI YA CLINIC YA MACHO
Love Tanzania Festival siyo tu itahusisha kuponya ROHO za watu kupitia neno la Mungu, pia watakuwepo Madaktari maalumu wa macho kutoka Marekani na watashirikiana na madaktari wa ki-Tanzania ambapo watakuwa wakipima watu mbalimbali wenye matatizo ya macho BURE, wale wenye matatizo ya kutoona vizuri maandishi watapewa MIWANI za kusomea BURE.Jumla ya miwani zipatazo elfu kumi(10,000) zipo kwa ajili ya kugawiwa kwa watanzania ambao watabainika na matatizo hayo, Ratiba ya Clinic hiyo itakayokuwa na vituo vinne ni kama ifuatavyo.

Kituo 1:St Nicholaus Anglican Church –ILALA
Kituo cha 2:Tanzania Assemblies of GOD (TAG-Mbagala)
Kituo cha 3:Lutheran Chuch – Vingunguti
Kituo cha 4: Baptist Mission Church – Magomeni

Kliniki zote hizi zitakuwa zinaanza saa nne asubuhi mpaka saa kumi jioni

Donnie Moen kuhudumu

Monday, July 30, 2012

My Heart Aches for 'Deceived' America- Billy Graham


The Rev. Billy Graham has posted a new prayer letter on his website where he addresses the people of the nation and tells them he is very much afraid of the damage that the American lifestyle is doing in the eyes of the Lord.

The 93-year-old evangelist begins his letter by recalling an incident a few years ago when his wife, Ruth, who has since passed away, remarked that "If God doesn't punish America, He'll have to apologize to Sodom and Gomorrah," referring to the cities in the Old Testament destroyed for the sinful nature of their residents.

Billy Graham
"I wonder what Ruth would think of America if she were alive today. In the years since she made that remark, millions of babies have been aborted and our nation seems largely unconcerned. Self-centered indulgence, pride, and a lack of shame over sin are now emblems of the American lifestyle," Graham remarks.

The pastor then goes on to refer to several other incidents in recent times where he sees the American government and American society as a whole coming down on Christians – including instances where chaplains who serve the police department have been told to no longer say the name of Jesus during prayer.

"Our society strives to avoid any possibility of offending anyone – except God," Graham says. "Yet the farther we get from God, the more the world spirals out of control."
"My heart aches for America and its deceived people," Graham continues. "The wonderful news is that our Lord is a God of mercy, and He responds to repentance. In Jonah's day, Nineveh was the lone world superpower – wealthy, unconcerned, and self-centered. When the Prophet Jonah finally traveled to Nineveh and proclaimed God's warning, people heard and repented."

Despite the critical condition he sees America in today, Graham shared that he still sees hope in the future, and believes that the people still have a chance to repent and change their ways. Sharing of future plans for his ministry, he described a project his son Franklin Graham will be working on – launching an outreach called "My Hope with Billy Graham," which has the mission to bring the Gospel into every neighborhood in America next year. The outreach effort has already reached more than 50 countries around the world.

"We've worked in close partnership with local churches across each country, and those churches have reported millions of life-changing decisions for Christ. Carrying out a nationwide American version of this evangelistic outreach will be an enormous undertaking, but in my spirit I know God has called us to do this, and I pray He will stir your heart to join us in prayer and support," Graham explained.

Sharing of his summer activities, the preacher noted that he is enjoying visits from his family and grandchildren, but that he is also working hard on a new book that outlines the path toward eternal salvation so that the world can wake up to what the Bible says.

"Although age and health restrict my mobility and my stamina, not to mention my eyesight and hearing, I am thankful for the days God has given me, and I am humbled by His continued hand of favor on the Billy Graham Evangelistic Association. The Lord draws people to Himself daily through BGEA's various evangelistic ministries, and I am so deeply grateful," Graham concluded.

Thursday, July 12, 2012

Coctail ThankGiving Night ya Uncle Jimmy Temu Kurindima Tamaal Hotel


Jimmy akiwa Redion
Waswahili walitangulia na Kusema UJANA MAJI YA MOTO na ni Ki-Mungu kumtumikia Mungu siku za UJANA kabla hazijafika siku utakazokuja kusema kuwa siwezi.Man of GOD James Temu ni kijana na  Mtangazaji wa kituo cha Redio cha Kikristo Kiitwacho Praise Power cha JIJINI Dar es Salaam, pia Jimmy  ni Mcheza Filamu maarufu nchini na on top of it  Uncle Jimmy kama ajulikanavyo na wengi ni mmoja kati ya ma-blogger mahiri wa habari za wa Kikristo nchini Tanzania.

Mwaka jana mwezi wa saba James Temu alianzisha blog yake iitwayo www.unclejimmytemu.blogspot.com na mwaka huu anatimiza mwaka mmoja katika kuielimisha jamii kwa habari ya ufalme wa Mungu kupitia mtandao.Hivyo basi kwa kuliona hilo gentleman huyu mrefu mweupe mwenye sauti nyembamba ameamua kuwaalika wadau wote kwenye Coctail Party maalumu ya kumshukuru Mungu kwa kumuwezesha kutimiza mwaka mmoja.

Jimmy akiwa katika harakati za kucheza Filamu pamoja na Ray na Waridi
Shughuli nzima itafanyikia tarehe 20.07.2012 katika Tamaal Hotel iliyoko maeneo ya Mwenge nyuma ya kituo cha Polisi, katika usiku huo marafiki ndugu na jamaa watapata nafasi ya kumfahamu Jimmy alikotoka alipo na mataraji yake  ya hapo baadaye.Muda ni kuanzia saa 1:00 usiku mpaka 3:00 usiku kiingilio ni BURE.Kama uko Dar es Salaam hii si ya kukosa fika Tamaal na tuseme EBENEZER pamoja na mwanahabari huyu.

Sambamba na Kumfahamu Jimmy,kwa kila atakayefika atapata nafasi ya kumtukuza Mungu LIVE pamoja na Live Band kutoka kwa Dar es Salaam Gospel Band pamoja na wanamuziki wengine maarufu nchini.Katika usiku huo chakula kitatolewa bure kwa kila atakayefika ambapo watangazaji wengi maarufu nchini watakuwepo katika kumshukuru Mungu pamoja na mwanahabari mwenzao.Kwa ROHO SAFI tukutane pale Tamaal Hotel ijumaa ya wiki ijayo(20.07.2012) tuseme EBENEZER pamoja na James Temu.

Jimmy akiwa ndani ya Friends on Friday White Party ambapo ni mmoja kati ya waandaaji wake

Wednesday, July 11, 2012

Anayetuhumiwa Kuvamia Kanisa La KKKT Iringa Afikishwa Mahakamani




Pichani ni Lawarance Mtatifikolo (30) Mkazi wa Image wilayani Kilolo, mkoani Iringa ambapo jana mtuhumiwa huyo Mtatifikolo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Mjini Iringa akituhumiwa kufanya fujo kinyume cha sheria ya makosa ya jinai kifungu namba 170 cha Kanuni ya Adhabu.

Katika mahakama hiyo ilielezwa kwamba mnamo Julai 8, mwaka huu , Mtatifiko akiwa na wenzake wanne (hawajakamatwa) walifanya kitendo kisichoruhusishwa kisheria kwa kufunga mlango wa kanisa na kusababisha usumbufu kwa waumini.

Walifunga lango kuu la kuingilia Kanisa Kuu la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Iringa wakilenga kufikisha ujumbe kwa Askofu wa Dayosisi hiyo kwamba hawataki aendelee kuwa kiongozi wao kwasababu anatuhuma nyingi za kimaadili na uongozi.

Kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Festo Lwila itatajwa tena mahakamani hapo Julai 24 wakati uchunguzi wake ukiendelea

Tuesday, July 10, 2012

Pastor Myamba Na Dhana Nzima Ya Uhalisia Katika Uigizaji


Mr Emmanuel Myamba ni mtumishi wa Mungu,ameokoka na anasali katika kanisa la Living Water Kawe Makuti lililo chini ya Mtume Onesmo Ndegi.Tofauti na utumishi Myamba ni muigizaji wa Filamu maarufu nchini Tanzania.katika moja ya washa aliwahi sema kuwa “Ni wazi ukiangalia filamu zetu zinakosa weledi katika uandishi wa miswada, uongozaji, uhariri na hata uumbaji wa wahusika. Lazima tukubali udhaifu huu turekebishe”  aliendelea kueleza kuwa “Nimekuwa katika tasnia ya filamu kwa muda sasa lakini kuna changamoto nyingi katika tasnia ya filamu, na jambo ambalo nimeliona ni wasanii kukosa ujuzi kitaaluma katika utendaji wa filamu kwa ujumla, kwa mantiki hiyo nikaamua kufungua chuo hiki kwa ajili ya wasanii maskini wasio na uwezo wa kulipa ada kubwa katika vyuo vilivyopo, lakini pia kutoa nafasi kwa wale ambao wanafanya kazi lakini taaluma imekuwa shida kwao, na mwito ni mkubwa kweli,”


“Tatizo kubwa la wasanii wa Tanzania kushindwa kufaidika na vipaji na ujuzi wao, ni kukosa elimu ya kutosha ya mambo ya sanaa, kwa mantiki hiyo nikaamua kufungua chuo hiki kwa ajili ya wasanii, nimeapa kwamba nitaweka ada ndogo ili wasanii wachanga au kwa ujumla tuseme wasio na uwezo mkubwa wa kifedha waweze kusoma hapa,”

Kati ya waigizaji wanaoigiza kwa hisia na kuvutia nyoyo za mashabiki hapa Tanzania basi hutakosa kumtaja Emmanuel Myamba a.k.a Pastor Myamba ambaye mara nyingi tumezoea kumuona akiigiza kama mchungaji au mtu mwenye maadili ya dini.



Mimi kama mdau  ninamkubali sana msanii huyu hasa katika kipaji chake cha kuigiza katika hali ya uhalisia wa maudhui ya kidini na kweli amefanikiwa kuvaa uchungaji wa kweli ambao ni zaidi ya movie wakati ni movie tu. Kutokana na kipaji hicho na umakini wa uigizaji wake wadau wengi tunajua kuwa Myamba ni mchungaji ambaye anakanisa lake, lakini kumbe sio, yeye ni mwigizaji na muumini wa kawaida tu. Hali hii sis wadau wa filamu ndio tunatamani kuangalia filamu zenye uhalisia wa namna hii. Katika kundi hili wasanii kama Dr. Cheni, JB, Wema Sepetu na Shamso Ford ni baadhi ya waigizaji ambao wanakuwa makini katika katika uigizaji wao;unaweza kufurahi nao au kulia nao ukifikiri kile kinachochezwa ni ukweli mtupu, kumbe sio ni filamu tu.

Swali ninalojiuliza hapa nini ambacho kinakosekana kwa wasanii wengi hata wale waanzilishi wa Tasnia hii? je tatizo ni nini? Je ni kweli swala la elimu linachangia kama?

Pastor Myamba alivyoshauri kuwa  “ni vyema kupata elimu kwani elimu inakufanya ujiamini juu ya unachokifanya na kwa umakini zaidi”.


Nina Imani kuwa kusaka maarifa ya namana ya kutengeneza sinema zenye uhalisia na visa litasaidia sana kuleta ushindani sio tu wa ndani bali wa limataifa; ikumbukwe kuwa filamu ambazo zinakosa uhalisia zinapunguza mvuto, na hivyo kuwafanya watazamaji kuishiwa na hamu ya kuziangalia filamu hizo na kuwakosesha kipato na kuongeza umasikini miongoni mwa wasanii.

Kama Gayo alivyowahi kushauri kuwa “Ikiwa tutaendelea kutengeneza filamu zisizo na weledi, zenye visa vilevile na zenye kusukumwa na wasambazaji au haja ya kuchuma fedha za haraka tu watu watatuchoka na baadaye soko litakufa”.


Hivyo kilio cha elimu kwa wasanii kimekuwa ni kilio cha wadau wengi hapa Gayo anasisitiza kuwa “Pia wasanii na watendaji wengine wanapaswa kupatiwa mafunzo, kwangu mafunzo ndiyo kitu cha kwanza muhimu kwa mtu yeyote yule katika kumuongezea stadi zake za utendaji. Kwa jumla kuna upungufu mkubwa wa mafunzo ya fani mbalimbali za sanaa, ikiwemo filamu. Wasanii wengi wanajifunza kwa kuiga wenzao. Ingawa hii ni moja ya njia za kujifunza, tatizo lake ni kuwa huchukua muda mrefu na haina hakika kama kinachoigwa ni sahihi au la”.

Je ni kweli sekta hii ni ya watu ambao hawajasoma? Mimi ninasema hapana? Isipokuwa ni sekta ambayo wahusika wake baada ya kushika pesa kidogo hunogewa na hawataki kujiendeleza kwa kujipanua katika elimu ya uigizaji; na kwa hiyo ufanisi wa kazi umekuwa wa chini mno.

Msanii Myamba ametuletea changamoto nzuri ya kuanzisha chuo cha filamu Tanzania kuppitia chuo hiki wasanii wataweza kukabiliana na changamoto za uandaji wa filamu kwa wasanii kukubali kujiongezea ujuzi na masilahi bora.Kwa hiyo eneo hili la mafunzo linahitaji msukumo siyo tu wa kuongeza nafasi bali pia ubora wake.

Wazungu na kiingereza chao wanasema "Knowledge" comes from getting educated.
"Experience" comes from real life encounters. There is a famous saying that says.

"Experience is better than knowledge!" and "Experience is the Best Education In Life."

 Experience and knowledge go hand in hand.
Knowledge is important, because it makes you aware of what is around you. Knowledge also enables a person to become wealthy.

The more knowledge we have, the more advanced we can become. Education can give you a good job and assure you a secure future. The world needs knowledge to discover new things to help everyone.


Msanii kama kioo halisi cha jamii inayomzunguka, anatakiwa kuuvaa uhalisia wa fani yake ili Yule anayeamua kumwangalia aweze kufaidika na tasnia hiyo. Ili kufikia malengo stahiki, wasanii mmoja mmoja au kwa pamoja wakipata upeo juu ya haya, wataweza kutekeleza ipasavyo majukumu yao na kuwa msaada mkubwa katika kuielimisha jamii juu ya mambo mbalimbali.

Nachukua nafasi kumpongeza Msanii Emmanuel Myamba aka Pastor Myamba kwa kuliona hili na kuanzisha chuo cha kuwaelemisha na kuwapa ujuzi unaostahili wasanii wengine ili waweze kukabili changamoto za kufanya kazia zao kwa makini na kwa uhalisia unaotakiwa katika tasinia ya filamu nchini kuptia Chuo kinachojulikana kwa jina Tanzania Film Training Center (TFTC) kilichopo  Ubungo  Dar Es Salaam  ambacho hutoa mafunzo mbailimbali ya filamu,ikiwemo acting, directing, editing, production management,producing nk


Monday, July 9, 2012

Christina Shusho akosa Tuzo za Muziki wa Injili Barani Afrika.

Emmy Kosgei kushoto alihudumu katika tuzo hizo na nyimbo yake ya Ololo ilipata tuzo ya nyimbo bora

Mwanamuziki pekee wa Injili kutoka Tanzania aliyekuwa akiiwakilisha nchi katika tuzo za Muziki wa Injili barani Afrika Christina Shusho, juzi jumamosi 07.072012  hakubahatika upata tuzo yeyote katika kilele cha shindano hilo lililofanyika nchini Uingereza katika kanisa la EL SHADDAI INTERNATIONAL CHRISTIAN CENTRE.

Katika tuzo hizo mwanamama Christina Shusho alikuwa akiwania tuzo mbili,ya kwanza ni mwanamuziki bora wa kike wa nyimbo za injili barani Afrika na nyingine ni mwanamuziki bora wa injili ukanda wa Afrika mashariki na kati, ambapo katika kategori zote mwakilishi huyu wa Tanzania hakubahatika kuibuka mshindi.Hii ni mara ya pili kwa Tanzania kushiriki katika tuzo hizo bila kupata.Ukavu huu haumaanishi hatuwezi ila unatupa changamoto ya kufanya kazi ya Mungu kwa nguvu zaidi na ipo siku KITAELEWEKA since GOD is not a respector of a person,he respects his word.

EL SHADDAI INTERNATIONAL CHRISTIAN CENTRE ambapo tukio zima lilifanyikia jumamosi iliyopita

Washindi katika kila kategori ni kama ifuatavyo wenye rangi ya njano

ARTIST OF THE YEAR- EAST AFRICA
1.     Eko Dydda- Kenya
2.     Emmy Kosgei - Kenya
3.     Exodus- Uganda
4.     Christina Shusho- Tanzania
5.     Lam Lungwar- South Sudan
6.     Sarah K-  Kenya
7.     Dawit Getachew-Ethiopia
8.     Kambua-Kenya
9.     Willie  Paul- Kenya
10.Ann Marie Mutesi - Burundi

ARTIST OF THE YEAR- SOUTHERN AFRICA
1.     Patrick Duncan
2.     Solly Mahlangu
3.     Hlengiwe Mhlaba
4.     Ambani Ramaru
5.     Sfiso Ncwane
6.     Bakhe Dlamini
7.     Keke Phoofolo
8.     Thobekile Mkhwanazi
9.     Ntokozo Mbambo
10.Prince Mafukidze



Patric Duncan wa Joyous Celebration aliibuka mwanamuziki bora wa Injili kwa nchi za Kusini mwa afrika nafasi iliyokuwa ikiwaniwa na Uche wa Double Double

ARTIST OF THE YEAR- WEST AFRICA
1.     Gifty Osei– Ghana
2.     Skuulfoo- Ghana
3.     Frank Edwards-Nigeria
4.     Cwasi Oteng-Ghana
5.     Tosin Martins –Nigeria
6.     Eben -Nigeria
7.     Evangelist Ben and Felicia Awabi- Cameroon
8.     King Mensah- Togo
9.     Atorise Lanre- Nigeria
10.Nii Okai-Ghana
11.Psalm Ebube - Nigeria

ARTIST OF THE YEAR- CENTRAL AFRICA
1.     Dena  Mwana (Congo)
2.     Anne Marie Mutesi (Burundi)
3.     Eddy Mico (Rwanda)
4.     Mike  Kalambayi (Congo)
5.     Alain Moloto (Congo)
6.     Achalle (Cameroon)
7.     Ngeh Loveline (Cameroon)
ARTIST OF THE YEAR (Solo/Group) - USA/CANADA
1.     Judah Tabernacle Choir
2.     Anita Etta
3.     Josephine Atanga
4.     Yaw Osei-Owusu
5.     Ike Wilson
6.     Fred Obare

Emmy Kosgei akienda kuifata tuzo yake ya nyimbo bora ya injili barani afrika 2012 
Solly Mahlangu aliibuka mwanamuziki bora wa Injili barani afrika 2012


ARTIST OF THE YEAR- EUROPE
1.     Dina Kikala, UK
2.     Masterdon, Italy
3.     Daniel Idikayi, UK
4.     Atta Boafo, UK
5.     Iyobo Van Lierop- Holland
6.     Kelechy Ify, UK
7.     Rebecca, UK
8.     Allen Caiquo, UK
9.     Mahali Selepe, UK
10.Myco Chris, UK
AFRO JAZZ /INSTRUMENTAL MUSICIAN OF THE YEAR
1.     Swazi Dlamini (South Africa)
2.     Mbaki (Bostwana)
3.     Lekan Shobiyi (UK)
4.     Mike Aremu (Nigeria)
5.     Nathi Zungu (South Africa)
6.     Miller Luwoye (UK)



ALBUM OF THE YEAR
1.     Colours of Africa- Sonnie Badu (UK)
2.     Crown Him King-Israel Mosehla (South Africa)
3.     Blessing-Diana Hamilton (UK)
4.     Ololo -  Emmy Kosgei (Kenya)
5.     Skuulfoo- Chapter 1 (Ghana)
6.     Declaring his Name- Muyiwa and Riversongz (UK)
7.     Overflo-  Florocka (Akinwunmi Nathan Akiremi) (Nigeria)
8.     Prophecy-Ohemaa Mercy (Ghana)
9.     Mwamba Mwamba- Solly Mahlangu (South Africa))
10.I Believe – Rebecca (UK)

AFRO GOSPEL RAP (SOLO/GROUP) OF THE YEAR
1.     Preachers (Ghana)
2.     Princess Dolly (UK)
3.     Rooftop MCs (Nigeria)
4.     Royal Priesthood (Ghana)
5.     Kriss Ehh Baba (Kenya)
6.     Andrew Bello (UK)
7.     Lyrical Soldier (UK)
8.     Fifty 50 (South Africa)
9.     Kardy (Cameroon)
10.Chuka Royalty (UK)
SONG OF THE YEAR
1.     Psalm 23-Eko Dydda (Kenya)
2.     Siyabonga Jesu- Solly Mahlangu  (South Africa)
3.     Ololo – Emmy Kosgei (Kenya)
4.     God Dey Bless Me- Cwesi Oteng (Ghana)
5.     Only You be God- Muyiwa and Riversongz (UK)
6.     Born Champion – DJ Gosporella ft. J. Clique (Nigeria)
7.     Champions- Tim Godfrey (Nigeria)
8.     Bless Somebody- Rebecca (UK)
9.     Minku Meho -Celina Boateng (Ghana)
10.Arabaribiti – Sonnie Badu (UK)

Benjamini Dube aliibuka na tuzo ya heshma

 
FEMALE ARTIST OF THE YEAR
1.     Emmy Kosgei-Kenya
2.     Dena Mwana – Congo
3.     Ntokozo Mbambo- South Africa
4.     Rebecca- UK
5.     Gifty Osei- Ghana
6.     Kefee -Nigeria
7.     Onos Ariyo- Nigeria
8.     Diana Hamilton-UK
9.     Christina Shusho -Tanzania
10.Lara George- Nigeria
MALE ARTISTE OF THE YEAR
1.     Solly Mahlangu-South Africa
2.     Eko Dydda-Kenya
3.     Frank Edwards- Nigeria
4.     Daddy Owen- Kenya
5.     Keke Phoofolo- South Africa
6.     Joe Praise- Nigeria
7.     Eben- Nigeria
8.     Uche- South Africa
9.     Allen Caiquo- UK
10.Aaaron T. Aaron- UK
EVENT OF THE YEAR
1.     Festival of Worship and Praise- (Italy)
2.     Joyous Celebration 16 Live Recording (South Africa)
3.     Evolution (Ghana)
4.     Crown Awards (South Africa)
5.     Groove Awards (Kenya)
6.     Talanta Awards Africa (USA)
GROUP/CHOIR OF THE YEAR
1.     Maximum Melodies- Kenya
2.     Simply Chrysolite-South Africa
3.     Makoma- Holland
4.     Tim Godfrey and Extreme Crew-Nigeria
5.     Skuulfoo-Ghana
6.     Vining Ogu and This Experience Choir - Nigeria
7.     Obert Mazivisa and the Trumpet Echoes
8.     Sowetos Spiritual Singers-South Africa
9.     Adawnage- Kenya
GOSPEL TV PROGRAM OF THE YEAR
1.     Le Chemin Des Artistes (UK)
2.     X2D (Nigeria)
3.     Crossover 101 NTV (Kenya)
4.     House of Praise (South Africa)
5.     Footprints (Ghana)
6.     One Gospel (South Africa)