Home

Friday, October 26, 2012

Benjamini Dube kuzindua DVD ya Healing in his Presence mnamo tarehe 10/November/2012





Album Cover ya Healing in His Presence na Dube anaonekana vizuri hapo pichani

Mwanamuziki na mtumishi wa Mungu mashuhuri nchini Afrika ya Kusini Benjamini Dube mnamo tarehe 10.11.2012 katika ukumbi wa Esibayeni Lodge, atakuwa akizindua DVD album yake mpya na inayofanya vizuri kwa sasa ndani na nje ya nchi hiyo iitwayo‘Healing in His Presence’ 

Akiongena na waandishi wa habari nchini Africa ya kusini siku mbili zilizopita Dube alisema kuwa yeye hana chcochote cha kuwaahidi watu watakaofika ila ana uhakika na uwepo wa nguvu za Mungu katika Ibada hiyo ya uzinduzi.Katika uzinduzi huo Dube atsindikizwa na Judith Sephuma, Margaret Motsage, Neyi Zimu, Nhlanhla Mdluli, PU2MA pamoja na watoto wake wa damu hapa namaanisha  kundi la “Dube Brothers” ambao ni  Mpho, Sihle pamoja na Buhle.

Mwanamama Judith Sephuma
Benjamini Dube afahamikaye kwa upole na unyenyekevu alizidi kusema kuwa “ Naamini siku hiyo Mungu atawabariki watu wote watakaofika kwa kuwa hawezi kuwaita watu waje pasipo sababu”. Kwa mujibu wa Dube Healing in His Presence ni moja kati ya Album ambazo yeye binafsi anazipenda sana na humo ndani amewashirikisha pia wanamuziki wenye vipaji akiwemo mwanadada Judith Sephuma.Hii ni album ya 15 toka Dube alipoanza kufanya muziki, Kiingilio katika uzinduzi huo kwa viti vya kawaida ni Sh za Kitanzania 27313.28/= (Randi 150) na VIP ni Sh 36417.70 sawa na Randi 200.

Dube alizidi kusema kuwa pamoja na kuwa yeye ni baba mzazi wa watoto wake “Dube Brothers(Mpho, Sihle pamoja na Buhle) huwa anaamini kuwa yeye ni Baba na mentor wa watu wengi duniani hususani katika Music Industry.Benjamini Dube alirejea nchini Africa ya Kusini Jumatatu iliyopita akitokea Zimbabwe ambako alienda mahususi kwa ajili ya kuinadi album yake hiyo na kuandaa mazingira ya Show yake nchini humo.


No comments:

Post a Comment