Home

Wednesday, October 3, 2012

Hatimaye Khaya Mthethwa wa JOYOUS Celebration atwaa SA Idol



Khaya Mthethwa akiwa stejini 

Awa mweusi wa kwanza kushinda katika shindano hilo toka lianzishwe mwaka 2002.
Apata randi 1m  sawa na shilingi za kitanzania 188,347,073.37na record deal
Unabii wa Pastor Ucheagu(My god id good ooh) kuwa nchi ya south Afrika isubiri mambo makubwa kutoka kwa Khaya wakumbukwa.

Khaya Mthethwa kijana kutoka kundi la Joyous celebration siku ya jana alitawazwa rasmi kuwa mshindi wa shindano la vipaji vya kuimba nchini Africa ya kusini maarufu kama South africa Idol series 8.Khaya mwenye miaka 25 ni mweusi wa kwanza kuchukua tuzo hiyo toka mashindano hayo yaanze mwaka 2002.Khaya mkazi wa Durban alikuwa akichuana kwa ukaribu kabisa na binti wa kizungu mwenye miaka 23 aitwaye Melissa.

Licha ya support kubwa aliyokuwa akiipata kutoka kwenye kundi lake la Joyous, umaridadi wake wa kuimba pamoja na kupiga kinanda kwa umahiri vilikuwa ni vitu vilivyombeba Khaya katika mashindano hayo.Haikuwa rahisi kwa Khaya kushinda kwani ushindani ulikuwa mkubwa, katika hatua iliyoonekana wazi kuwa raia weusi wa Africa ya kusini wanamkubali Khaya, wengi wao iliwabidi wanunue kadi mbili mbili ilimradi tu wampigie kura nyingi.

Khaya Mthethwa akiwajibika jukwaani
Ikumbukwe kuwa kura zilikuwa zikipigwa kupitia channel za kulipia(subscription chanels) ambazo kimsingi inakubidi ununue kadi za kukuwezesha kuona na ku-vote. Kwa upande mwingine upigaji huu wa kura uliwapelekea wengi wa mashabiki wa Khaya hususani wenye kipato cha chini kushindwa kupiga kura.Wakati wa mashindano hayo Khaya aliwahi imba nyimbo ya Nick Minaji - Super Bass

Khaya Mthethwa akiwa na mpinzani wake Mellisa wakati wa mchujo  
Kwa ushindi huo Khaya ameondoka na kiasi cha randi R1m ambazo ni sawa na Paundi £74,139 zenye thamani ya kiasi cha shilingi za Kitanzania 188,347,073.37.Khaya ambaye ameanza kuonekana na kundi la Joyous Celebration katika album yao ya 15 na kumi 16, aliwahi pewa neno la Kinabii na mwanamuziki mwezie Pastor Ucheagu kuwa nchi ya south Afrika isubiri mambo makubwa kutoka kwa Khaya.Wengi wa wana-joyous na ex-joyous akiwemo Nthokozo wamempongeza Khaya kwa mafanikio haya.

Khaya Mthethwa akiwa na Mnthunzi Namba  katika Joyous 15  
Kwa mujibu wa website ya Khaya, klhaya alianza kupiga drums akiwa na umri wa miaka kumi na hii ilikuwa ni kati ya mwaka 2001-2003 kiasha akaamua kwenda kwenye chuo cha kufundisha Sauti(Vocal training).Tofauti na kupiga drums, Khaya ni mahiri katika kupiga gitaa,na keyboard pia ni worshiper ,song writter na music director katika kanisa analoabudia.

Chukua hii:Kwa Tanzania Praise leader wenu akishiriki BONGO STARSEACH usishangae akitengwa.


No comments:

Post a Comment