Home

Thursday, October 4, 2012

Kanisa linamtazamo gani juu ya Vijana wa waliookoka wenye vipaji vya Uanamitindo (Modeling) !!



Felix Mshama
Kwa mara ya Kwanza nakutana na Felix Mshama ilikuwa ni usiku tukiwa chuoni SAUT ndani ya Fellowship TAFES, akiwa First year mi hapo ndo 3rd year nkashangaa huyu dogo mtata kafika Juzi tu chuo leo Fellowship anapiga gitaa!!, pembeni  walikuwepo wapiga vyombo wakongwe wanapiga jaramba.

Baada ya fellowship nkamfata akaniambia anatokea Dodoma  na anachukua degree ya sheria na ni mtoto wa mchungaji, then tukapiga story mbili tatu nkagundua dogo sio tu GITAA, anaweza akafanya Medeling(Uanamitindo).Sikusita faster nkamuuliza mtumishi  ulishawahi fanya Modelling? akasema Bro umejuaje!! Ki-Ukweli sijawahi but hiyo ni moja kati ya dream zangu, na tokea hapo tulipokuwa tukikutana nilimwuita TAFES-MODO.

Man of GOD Felix Mshama
Baada ya semister ya kwanza kuisha, TAFES-SAUT ili-organise Evangelism Mission chini ya MAMBO MAKUYA na hapo tulienda kijiji cha GAMBOSI kwa lengo la kumtangaza Kristo katika kijiji hicho kinachosifika Afrika Mashariki na Kati kwa imani za Ushirikina.Huko tulienda wengi zaidi ya wanachuo hamsini.Tukiwa Gambosi time table ilikuwa tight sana na kila mtu alikuwa ROHONI ile mbaya kwa kuwa tulitaniana kuwa ukicheza utaacha shingo Kiwiliwili kirudi kumalizia Bachelor Degree.

Nakumbuka kila siku jioni tulienda kuonyesha Sinema, kwa kuwa nilikuwa mmoja wa ma IT nilitakiwa kuwahi kuweka mambo sawa, siku moja nlimchukua dogo(FELIX) kisha mdogo mdogo na Itatiro, Humphrey na Alex tulielekea uwanjani.Tukiwa njiani nlimuuliza MODO(Felix) ntupie Ma-cult work zaidi Jokate na Magese.Hahaaaa akasema ngoja nikupe Intro ndipo  akaanza kutembea kwa umaridadi as a model kifupi dogo alitisha.

Felix Mshama akiwa na Noel Mlabwa pamoja na Barnabas shija katika video yao mpya iitwayo UMWEMA
Kikubwa nachojiuliza kwa Vijana waliookoka  kama FELIX, hizi Talents zao za Modelling na nyingine wanaweza wakazionyesha wapi!!, na kimsingi ni AJIRA, tukisema wakakae chini ya madesigner kama Ally Remtullah,Khadija Mwanamboka, au Mustapha Hasanali (Slim Slim),  ipo siku wataaambiwa wavae nusu uchi, na wakirudi kanisani wanaambulia kutengwa. 

So youth wafanye nini, wafe na Talent zao, au wachague nguo za Kuvaa!!! Kitu ambacho kwa ma-designer sio rahisi. Finally utagundua kuna vitu vingi vimepungua katika jamii ya Kikristo nchini, kwa sasa Nadhani we need CHRISTIAN MODELLING AGENCIES zitakazofanya Modelling huku ziki-preserve PURITY in Christianity.

Hapa chini ni moja kati ya kazi ambazo Felix Mshama aliifanya akiwa na wenzie Noel na Barnabas

Video Imefanywa na Kinye-Media

Gitaa limepigwa na Felix



1 comment: