Home

Friday, November 2, 2012

Kanisa la Waadventista(Wasabato), lapitisha azimio la kupinga kuwaapisha wanawake


Makamu wa Rais wa Kanisa la Wasabato Ulimwenguni Mtumishi Lowell Cooper akisoma waraka wa maafikiano ya kikao hicho mara baada ya kura kupigwa

Kanisa la waadventista wasabato ulimwenguni katika kikao chake cha mwaka mwishoni mwa mwezi uliopita, limepiga kura za kupinga uwekwaji wakfu kwa wanawake kitendo kilichofanywa na union tatu za kanisa hilo.Union  zilizopitisha hatua hiyo ni za Ujerumani kaskazini, Columbia na Pasifiki,Union hizo zilipitisha mabadiliko hayo hivi karibuni. 

Kufuatia mjadala wa masaa 3, kanisa la SDA Duniani  limekuja na waraka ukizitaka union hizo kuacha mpango wao huo na kubaki katika umoja katika kristo, kama alivyokaririwa Mch Ted wilson akisema "focusing on the mission of the Church, uniting in Christ, even though we will face some differences and disagreements.". Kura 264 dhidi ya 25 zilikataa kuapisha wanawake.

Sehemu ya wajumbe wa kikao hicho

No comments:

Post a Comment