Nkhululi Bhebhe aongelea Uwepo wake Joyous Celebration
|
Nkululi Bhebhe |
Kwa wadau wanaolifuatilia kwa ukaribu kundi la Joyous Cerebration Jina la Nkululi Bhebe sio jina geni masikioni mwao.Bhebhe ambaye ni raia wa Zimbabwe, amukuwa akifanya vizuri ndani ya kundi hilo toka alipojiunga nalo akitokea Zimbabwe mwaka 2010. Alipo-lead katika nyimbo ya Tambira Jehova kwenye Joyous 15 ndipo alipokuwa gumzo katika vinywa vya wapenzi wengi wa kundi hilo.
Hivi karibuni Bhebhe alifanya mahojiano na Jarida la Standard Life&Style la nchini Afrika ya Kusini alisema, anafurahia sana uwepo wake ndani ya kundi hilo, akaendelea kusema na hapa namnukuu
|
Joyous Celebration |
“Kwa sasa nimeshazoea mazingira yalivyo ndani ya kundi na mashabiki,kwa sasa mimi sio mgeni tena Joyous kama ambavyo watu walikuwa wakinichukulia. Mwaka 2011 uliikuwa mwaka wenye changamoto nyingi sana kwangu na ni mwaka ambao kundi letu lilipata nafasi ya kufanya Ziara nchini kwetu(Zimbabwe) na pia lili-record album mbili ndani ya muda mfupi.Nafurahi kwa kuwa wakati hayo yanatokea nilikuwemo ndani ya kundi.”
“Wakati wa ziara yetu nchini Zimbabwe, Wengi wa wanakwaya wenzangu ilikuwa ni mara yao ya kwanza kukanyaga Ardhi ya Zimbabwe, na mpaka leo wanaongelea uzuri na ukarimu wa watu wa Zimbabwe waliouonyesha kwetu kwa kipindi tulichokuwa nchini humo”
|
Joyous Celebration |
Katika Joyous 16 inayotarajiwa kutoka muda wowote baada ya kurekodiwa LIVE mwishoni mwa mwaka jana,Nkululi Bhebhe amelead(ame-solo) kwenye nyimbo inayoitwa “Usarambe Kudaira.”
“Mungu amekuwa mwaminifu sana kwangu kwangu kwa kipindi chote nikiwa Nchini Afrika ya kusini, na idadi ya mashabiki wangu imeongezeka zaidi ya nilivyokuwa nikifikira.Na kwa hili nimetambua kuwa sio mimi niliyoyafanya haya, isipokuwa ni Yesu aliye ndani yangu” alimalizia Bhebhe.
No comments:
Post a Comment