Saturday, August 13, 2011

Ushuhuda: wapata mtoto baada ya maombi ya muda mrefu.

 

Bwana Yesu Asifiwe sana.

Sisi tunaishi Dar, na tumekuwa wahudhuriaji wa semina  zote ambazo Mwl Christopher Mwakasege anazokuja kufundisha hapa Dar, japo si kwa siku zote za semina bali siku chache kwa kila semina, huwa tunapata angalau siku mbili,tatu. Tumebarikiwa sana na vitabu vya mafundisho mbalimbali.

Tunamshuhudia Mungu mwaka 2008, kwa kupitia mafundisho ya kitabu cha kumiliki na kutawala kwa njia ya maombi ambacho kinafundisha mbinu za kufaya maombi ya muda mrefu, hakika tulifanya kazi mafundisho hayo na hatimaye Roho Mtakatifu alitufundisha na kutuwezesha kufanya maombi ya muda mrefu ambayo hatujawahi kuanya katika maisha yetu yote.

Tulikuwa na hitaji letu tulilokuwa tunamweleza Mungu na hatimaye, Mungu alitujibu na kutupa mzaliwa wa kwanza(lango la familia).
Katika maombi haya , tulijifunza sana mambo mengi na kugundua kwamba ,maombi ya muda mrefu yana siri kubwa sana ya mafanikio ambapo Mungu hujidhihirisha dhahiri kwa yote umwombayo.Jina la Bwana liinuliwe juu.

Tumejifunza kwamba kitu kizuri huwa na vita sana, ili ukate tamaa ya kuomba (kuachilia nguvu za Mungu kwa kiwango kikubwa) sawa sawa na uzito wa jambo husika.
 
Kwa hiyo, uvivu na uzito wa kusoma vitabu vya mafundisho, biblia, kuomba na kushindwa kuomba kwa muda mrefu ni mbinu atumiazo adui akijua dhahiri kuwa katka maombi hayo,kuna mafanikio makubwa,ya kudumu na ya muda mrefu .

Ni maombi yetu ,watumishi wa Mungu muwe na afya njema na mafanikio zaidi ya kiroho na kimwili pia ili mwendelee kulisha kondoo wa Bwana.

MR & MRS.Wilson Shoo.

Taarifa: Hosanna Inc inapokea Shuhuda mbalimbali za matendo makuu ya Mungu ambayo amefanya kwa watu mbalimbali iwe ni kwako , rafiki, ndugu au jamaa kwa Utukufu wa Mungu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...