Wednesday, August 3, 2011

ASKOFU MTOKAMBALI ASEMA VYAMA VYA SIASA HAVINA MAJIBU KWA WATANZANIA.

Dr Barnabas Mtokambali
Askofu mkuu wa kanisa Assemblies of God [TAG], Dr Barnabas Mtokambali amewataka watanzania kufahamu kuwa majibu ya matatizo waliyonayo hayawezi kutatuliwa na vyama vya siasa, kutokana na kwamba wanasiasa wengi wapo kimaslahi yao wenyewe, badala yake amewahimiza kutambua kuwa majibu yako kwa Mungu pekee.
           
Rai hiyo aliitoa week iliyopita katika kanisa la  TAG Basihaya lililo nje kidogo na mji wa Dar es saiaam na  linaongozwa na mchungaji  Michael Salaka , Dr Mtokambali aliyasema hayo  alipofanya ziara ya kichungaji katika sehemu ya mbezi Bunju na Bagamoyo, ambapo alisisitiza juu ya watu kuondokana na dhana kwamba chama Fulani cha siasa kina uwezo wa kuondoa changamato mbambali zinazowakabili.
           
Kiongozi huyo wa kiroho alisisitiza kuwa, watanzania wanatakiwa kutambua kwamba wanapokabiliwa na matatizo makubwa yasiyo na majibu wana paswa kumtazama Yesu kristo nasi vinginevyo.
           
“Jibu la Tanzania haliko CHADEMA, CCM, wala katika chama kingine chochote cha siasa, liko kwa Yesu pekee, wanasiasawengi wanaganga njaa, hata hao wanaochaguliwa, tofauti yao ni kwamba huenda yeye anakula kidigo ukilinganisha mwingine”  
                
Sambambana hilo alisema kwamba, kanisa la Mungu linatakiwa liwe ndilo chombo kinachoweza kuwaondolea watu shida zao mbalimbali, kama ilivyo kuwa nyakati za Bibilia, ambapo alioongezea kuwa, hata majanga mengi yanayo ibuka kila kukicha ni nkutokana na watu wa Mungu kutosimama katika zamu zao.
                 
Alisema kuwa, watu wengi wenye ulemavu wa ngozi, wamekuwa wakionewa na watu wenye uchu wa mali kiasi cha kutoa uhai wao wakati wapo watu waliookoka.
                  
“Inauma sana kuona kuna watu wanachunwa ngozi zao nawengine kuuawa  kikatili, sambamba na watoto kufanyiwa matedo yasiyo ya hiyana na wazazi wao kabisa, wakati kanisa lipo na linaangalia,” alisikitika Dk. Mtokambali.
                   
Hata hivyo Askofu Dk. Mtokambali akiongelea juu ya suala zima la kufunga mbele za Mungu, alisema kuwa kuna aina nyingi za kufunga, lakini katika yote mtu akitaka kufunga siku 40, lazima iwe imetoka kwa Mungu mwenyewe nasio kukurupuka tu.

Sambamba na hilo Askofu Mtoka mbali nakizidi kueleza zaidi katika ibada hiyo maalum alisema kwamba, nchi za kiarabu sasa hivi zipo kwenye mapinduzi makubwa ya kisiasa, ambapo alibainisha kwamba kanisa nalo kwana mna moja au nyingine ni lazima lifanye mapinduzi ya kuondokana na kila aina ya dhambi, ikiwa ni pamoja na kutafuta kuwa watakatifu.
                     
 “Kanisa linatakiwa kubaki na maono ya matendo ya mitume, lazima tutafute kuwa watakatifu … Wachungaji, Maaskofu waangalizi, waumini wakati umefika wa kuingiwa na wivu wa Bwana. Utakatifu hufanya mtu kuinuliwa,” alisisitiza. 


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...