Tuesday, November 15, 2011

Nini Cha Kufanya Mungu Anapoweka Msukumo Wa Kuomba Ndani Yako? (Part 2)


Kumbuka lengo la ujumbe huu ni kukusaidia ili maombi yako yawe ni maombi yenye matokeo mazuri. Maana kama ni kuomba huenda umeomba sana lakini huoni matokeo ya maombi yako. Na suala si kuomba tu, unaweza ukaomba kwa muda mrefu na kufunga lakini kama hatuoni matokeo ya maombi yako haitusadii kwa lolote na haikusaidii pia kwa lolote. 


Mambo yafuatayo yatakusaidia kuboresha maombi yako ili yawe na matokeo mazuri zaidi, fuatana nami katika sehemu hii ya pili;

 Namna ya kuomba kwa kuzingatia mfumo wa kuombea unachokiombea;
1 Yohana 5:14 “… Kama tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake”. Je Kuomba huku kukoje au ni kwa namna gani?
 • Kuomba kwa uongozi wake (Roho Mtakatifu),i.e kwa kuzingatia maagizo yake. Waefeso 6:18 “Pray in the Spirit”.
 • Kuomba kwa kuzingatia upako wa Mungu ulioko juu yako.
 • Kuomba kwa imani katika Jina la Yesu (Yohana 14:13, 16:23, Matendo 3:16).
 • Kuomba wakati moyo wako haukuhukumu (1Yohana 3:21-22).
 • Kuomba kwa kujenga hoja zenye nguvu.
 • Kuomba kwa juhudi na bila kukata tamaa, (Luka 18:1).
 • Kuomba kwa kuzingatia muda unaotumia kuliombea jambo husika. Na linapokuja suala la muda kuna tafsiri mbili. Moja unaomba kwa muda gani i.e kwa dakika au masaa mangapi?, mbili unaomba wakati gani yaani saa ile unaposikia msukumo wa kuomba au kwa wakati unaotaka wewe?, (Luka 18:1-8, Matendo ya Mitume 12:1).
 Hata hivyo suala sio kuomba tu, bali katika maombi yako zingatia yafuatayo;
 • Kwa nini uombe, unaombaje, na unaombea wapi?
 • Unaomba kwa muda gani?
 • Katika na kutoka nafasi ipi? yaani kama nani?
 • Ukiwa na ufahamu kiasi gani juu ya suala unaloliombea?
 • Ukiwa na ufahamu kiasi gani juu ya maandiko yanayohusu suala unaliliombea?
 • Ukilenga nini katika kuomba kwako?
 • Unaomba ukiwa katika hali gani kiroho?
 • Je unaomba huku ndani yako unaona nini? (Marko 8:22-26).
 • Omba kwa sala zote i.e kukiri, kuungama,kufunga,kusifu nk. (Waefeso 6:18).
 Bwana Mungu akubariki, naamini dondoo hizi chache za mwisho zinakamilisha somo hili la “nini cha kufanya Munguanapoweka msukumo wa kuomba ndani yako?” swali aliloniuliza kiongozi wa kiroho wa mkoa wa Lindi.

Weka kwenye matendo na jifunze kujiuliza maswali hayo kabla hujaomba naamini utaona mabadiliko kwenye maombi yako.

Neema ya Kristo ikulinde.
Na: Sanga,P.S.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...