Monday, November 5, 2012

Kwa Jimmy Gait kuchaguliwa kuwania Tuzo za Kora 2012, wanamuziki wa Injili kutoka Tanzania wanajifunza nini?


Jimmy Gait

Jimmy Gait ni mwanamuziki wa injili kutoka nchini Kenya, kwa muda sasa Jimmy amekuwa aki-make headline katika nchi zote za Afrika Mashariki na kati hususani pale alipotoa wimbo wake wa Furi Furi dance aliomshirikisha D.K.Wiki iliyopita Jimmy gait amechaguliwa kuwania tuzo za kora kwa mwaka huu wa 2012 katika kategori ya mwanamuziki bora wa kiume toka Afrika mashariki. Katika kategori hiyo mtumishi huyo atakuwa akichuana  sambamba na Ali Kiba-Single boy Feat Lady Jay Dee Tanzania , Kidum Feat Sana – Mulika Mwizi, Burundi, Redsan – Ila Wewe, Kenya, Chris D – Aisha, Burundi na Mulatu Astatke.

Kwa wanaomfatilia Jimmy Gait aliyetambulishwa vilivyo na nyimbo yake ya Huratiti,Muhadhara,Holy Day alomshirikisha Kambua, na the hit Dance Hall track iloitwa MANYUNYU alomshirikisha Mkongwe Rufftone. Ki-umbo na umri Gait ni bado bwana mdogo na  moja kati ya vitu vinavyomtofautisha na wanamuziki wengi ndani na nje ya nchi hiyo ni staili yake ya uimbaji na uchezaji. Siwezi sema Jimmy ana-copy idea za uimbaji na uchezaji wa bongo fleva toka Tanzania kisha yeye kuzichange na kuja na staili yake but creativity na njaa ya kutaka kufika mbali ni moja ya sababu zilizomfikisha hapo.

Maswali ambayo wanamuziki wa Injili toka Tanzania wanapaswa kujiuliza ni kuwa ikiwa Jimmy Gait kafika Kora, wao wako wapi? Na sina mashaka kuna wengine hata Jimmy Gait hawamjui but mtumishi ndo hivyo katusua KORA !!! at least mtumishi yumo kati ya wanaowania.Kwa Wanamuziki wengi wa Injili toka Tanzania wanaweza sema kinachowakwamisha ni connection, ooooh mtumishi sina connection swali linakuja umetafuta Connection au baada ya maombi na mazoezi ulienda kulala!! 

Ni wazi kwa sasa muziki na system ya Muziki imebadilika kama ishu ni connection mtumishi tafuta meneja au watu  wenye upeo kisha wafanye nao wajisikie kuwa ni sehemu ya huduma yako. Kama kuna eneo ambalo waimbaji wa gospel wanaliona lina mapepo ni wao kuwa na meneja au kutafuta Kampuni ya kuwa manage.

Jimmy Gait Gospel star mzaliwa wa Limulu 

Naposema meneja sina maana lazima awe anakumanage kifedha tu(anakupa fedha kadri unavyoitaji) NO!!, anaweza fanya hivyo but hapa namaanisha tafuta mtu mwenye upeo wa kuona mbele (International Wise) ambaye atakushauri kulingana na namna Muziki wa Injili ulivyo na jinsi gani unaweza peleka kazi zako au ukajitangaza Kimataifa.Kuwa na meneja au timu ya watu au kampuni hili linafanyika na still ni la Kiroho kabisa, kumbuka Isaka alipotaka kuoa alipewa direction nenda kwa wajomba zako, ukifika binti ambaye atakupa maji kisha .......Kwa kusema hivyo namaana  Isaka angeenda chaka kumpata Rebeka endapo asingekaa na watu(mtu) sahihi.

Nakumbuka nikiwa Mwanza mwaka jana 2011, kwa sehemu nilikuwa katika timu ya John Lisu katika kuhakikisha Jehova YU HAI TOUR inafanikiwa jijini humo.Nikiwa na baadhi ya wenzangu nilijifunza sana namna ambavyo John Lisu anafanya kazi.Huyu mtumishi unaweza fikiri yuko peke yake, laah hasha kuna timu ya watu ambao kwanza wanasikilizana katika kila movement anayopiga kuanzia Concert lifanyike wapi, kwa gharama gani, tunaenda na kina nani, promo( Samuel Sasali anaita fitna) zifanyike vipi na mengine mengi.Hapa utaona ili kufika mbali mwanamuziki huna budi kuwa na watu nyuma yako ambao kwa pamoja mta-share maono nao watakusaidia kufika kule Mungu anakotaka ufike.


Jimmy Gait ndani ya Single Button kwa hapa Tanzania lazima tungeamini Martin Kandida kahusika kumvisha

Wanamuziki wengi wa injili ukiwauliza maono yao watakwambia nataka kufika International level, kaa nao vizuri uwaulize wamejipanga vipi kufika huko unaweza cheka, siwakebehi ila nimekutana nao wengi hawana MBINU wana MTAZAMO. Labda niseme kwa staili hii naamini itaeleweka vizuri wanamuziki wengi wa Tanzania hawana MISSION bali wana wana VISION, sasa unaweza pata picha wako Dar wana taka kwenda Dodoma ila wana nauli ya kuishia Msamvu.

Kwa utafiti wangu nimegundua shetani anapiga vita sana wanamuziki wa injili kutoka Tanzania wasiwe na ufahamu Neno la Mungu na namna ya kufika International Level. kwa kuwa endapo Watanzania tutakaa sawa hapo tofauti na Africa ya Kusini NAAMINI hakuna nchi katika Africa inaweza kutufikia kiuimbaji.Kwa kuwa hata ukibisha nyimbo nyingi za kitanzania  zina upako wa viwango vya juu lakini upako huo unaishia kusikilizwa hapa nchini  pekee, ni wazi upako wetu hau-cross boader!!! Na hata uki-cross sio kiiiiivyo!!!.
Kama tunataka kufika International lazima tukubali mabadiliko, Utakuta kwaya inataka kufika International lakini kila album wame-shoot kwenye maua, shoots za Kanisani wakizidi sana porini kwisha, huwezi fikiria album tano walizowahi fanya zote mule mule then unataka kugusa KORA camoon hatufiki, huwezi piga msasa mkaa ukitegemea one day utafanana na mninga, na sio busara kukebehi video za kwenye bustani, mbele ya majengo makubwa nk kwa kuwa hizo ndizo zinazotupa HASIRA ya kufanya mabadiliko.Kwa waliofika Nairobi waulize, kule wanajua vilivyo habari ya Bonny Mwaitege lakini Bongo wanaomjua Jimmy ni wachache, tatizo sio kumfunika mwingine kwa kujulikana bali mwanamuziki jiulize wadau wanaonizunguka wanauwezo wa kunifikisha mbali?

Labda niweke wazi kwa ambao hawafahamu juu ya hili, ili nyimbo ifikie International Level Kama kwenye Tuzo za KORA, MAMA AFRICA, na  Chanel O ni lazima iwe na vitu kadhaa vya msingi. Kwanza ni ubora wa kazi ya Audio, pili ni ubora wa Video kwa maana ya Sauti, Rangi, Mwanga ,Location, Shoots na ubora wa story kama itatokea ndani ya video yako kuna story. Hizi ni basics tu vipo vitu vingi, ieleweke upeo wa mwanamuziki juu ya soko la muziki wake nje ya nchi ndio humpelekea yeye kulitafuta soko hilo.Jiulize leo ni kawaida kwa station za radio nchini kutopiga nyimbo za Ambwene Yesaya(A.Y), lakini jamaa yuko vizuri tu kwa kuwa kahamishia mtazamo wake mbele ndio maana haikunishangaza kuona mwaka huu kaingia kwenye kategori tatu za tuzo za Channel O, Wakati hao wanaojiita ma-supestar wa Bongo fleva nchini huwezi amini bado wanalipa bili .......... Fm Radio, ili tu  nyimbo zao ziendelee kupigwa japokuwa zinaimbwa sana na watoto mtaani.

Tukirudi kwenye eneo la wito wetu(Gospel), huwa nafarijika napoona waimbaji wa nyimbo za injili  walioko vyuoni au waliomaliza wakikaa sawa maeneo yote, kiuandishi, nidhamu  ya Mungu na professionalism kwani always hutaka kuwa na video na audio bora.Mabadiliko ya muziki wa Injili yanawategemea waimbaji pamoja na wewe na mimi tusio waimbaji.Kwa ajili ya kuujenga mwili wa Kristo hatuna budi kutazamishana mbali kwani inakuhitaji baiskeli tu kutoka ubungo kwenda Kimara, lakini kutoka Ubungo kwenda Mbeya lazima ubadili mtazamo baiskeli sio mahala pake.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...