Kundi
la kiisilamu la Boko Haram nchini Nigeria, na vikosi vya usalama, wote
wametuhumiwa na shirika la kimataifa la haki za binadamu la Amnesty
International kwa kufanya vitendo vya kukiuka haki za binadamu hasa katika eneo
la Kaskazini lenye waisilamu wengi.Boko Haram, ambalo jina lake linamaanisha
elimu ya kimagharibi imeharamishwa, kufanya harakati za kuiangusha serikali na
kuunda taifa la kiisilamu.
Wanigeria wakifanya maombi |
Taarifa
zinazohusiana zinasema Siasa Siku ya Jumapili, kanisa lilishambuliwa na
kusababisha vifo vya watu wanane mjini Kaduna, mojawapo ya miji ambayo
imeathirika kutokana na mzozo unaoendelea kati ya serikali na Boko Haram.Ingawa
hawajakiri kufanya mashambulizi hayo, kundi hilo limewajibika wakati
lilipofanya mashambulizi Kaskazini na kati kati mwa Nigeria.
Obadiah
Diji, kiongozi mmoja wa vijana wa kikristo mjini Kaduna, alisimulia BBC ambavyo
maisha yamebadilika mjini humo.“ watu wanaogopa hata kutoka nje usiku au hata
kukaa nje tu kunywa pombe au hata kula samaki. Nimeishi mjini Kaduna karibu
maisha yangu yote na nimejawa na huzuni sana nikiona ambavyo umegawanyika sana
kwa ,misingi ya kidini.
Waisilamu
wanaishi ambako idadi yao ni kubwa, wakristo nao vile vile. Kwa hivyo makundi
hayo mawili ya watu, yanaishi maisha yao kivyao bila kutangamanaSio kawaida
kuwa hivi. Wakati mmoja tulijivunia kwa sababu ya umoja uliokuwa unadhihirika
hapa Kaduna na kila mtu alikuwa anakaribishwa hapa.
Ingawa
kulikuwa na migawanyiko, wakristo na waisilamu waliishi kwa pamoja. Tulikuwa
tunatembeleana . Watoto wetu walisoma katika shule koja , wakijifunza kutoka
kwa kila mmoja kuhusu dini na tamaduni zao.
Moja kati ya Mauaji ya Boko Hatamu |
Watu
hata walioana licha ya dini zao mfano mamangu wa kambo alibadili dini na kuwa
muisilamu na kisha akaoa muisilamu. Dadangu pia aliolewa na muisilamu ingawa
alisalia kuwa mkristo. Kuna ndoa nyingi kama hizo mjini Kaduna. Haikuwahi
kusababisha tatizo lolote. Watu waliheshimiana na kustahimiliana , sio chuki
wala ghasia.Mambo yalibadilika mwaka 2000 wakati Kaduna ilishambuliwa kwa mara
ya kwanza na mzozo wa kidini ambao unachochewa na makundi yanayotaka sheria za
kiisilamu.
Hapo
ndipo makundi yaliyohisi kutengwa yalijitokeza. Watu walitoroka makwao kwa
sababu ya ghasia. Wakristo walijipata wakiishi katika eneo lao mjini kaduna
huku waisilamu nao wakijipata wakiishi maeneo yao.Nimekuwa nikipinga maeneo
yaliyotengewa jamii moja na ndio maana bado naishi na mke wake na watoto wetu
wanne katika eneo ambalo ni la waisilamu wengi.
Wanawake
katika mikutano kadhaa maeneo ya Kaskazini wamepigwa marufuku kubeba vibeti
kanisani. Makanisa mengi sasa yana vifaa vya kuwachungua watu wanaoingia
kanisani ikiwa wana silaha yoyote au la.Wanawake wanazuiwa kubeba vibeti kwa
sababu mshambuliaji anaweza kuingia kanisani akiwahadaa watu kuwa ni muumini
kumbe amebeba silaha kwenye kibeti chake.Kwa hivyo maisha yetu ya kidini
yameathiriwa sana pamoja na hata maisha ya kijamii.
Sasa
tunaishi maisha ya faragha muda wote tukikaa nyumbani. Ni polisi pekee ambao
wanapatikana barabarani usiku.Lakini ghasia zimewafanya watu kuwa na imani sana,
Wanapata imani hiyo kutoka kwa bibilia ambayo inasema tutapitia mateso kama
alivyoteswa Yesu .Ujumbe ambao sisi wakristo tunasambaza ni kwamba waisilamu ni
watu wazuri na ni wachache miongoni mwao ambao wanasababisha vurugu, hatapaswi
kuvuruga uhusiano kati ya jamii hizo mbili.
Wakati
waisilamu waliposherehekea Eid al-Kabir, tuliungana nao katika barabara moja
mjini , tulikula pamoja na kusherehekea ili kuimarisha makubaliano ya amani na
umoja.Kwa wakati huu, hata mizozo ya kisiasa inageuka na kuwa ya kidini. Siku
mbili baadaye, kanisa lilishambuliwa kwa mabomu lakini hilo halitasitisha
juhudi zetu za kupatana.
Shule za pamoja
Wakristo
na wasilamu husoma hapa na wao ndio tunawategmea kwa mustakabali wetu.Tunatumai
watakuwa na kusoma pamoja na kufahamu kuwa tunaweza kuwa watu wa dini mbali
mbali lakini bado tunaweza kuishi pamoja.Washambuliaji wa kujitoa mhanga,
wamekuwa wakilenga makanisa Kaskazini mwa Nigeria. Ili kupunguza vurugu katika
jamii lazima tudurusu mfumo wa siasa zetu. Tunahitaji kuuliza , je Nigeria
ilikuwa sawa kuanza kutumia mfumo wa demokrasia ya kimagharibi?
Wanawake waliopoteza jamaa zao kwenye
shambulizi la Boko Haram
Hata
hatukuwahi kuwa na kiwango hiki cha ghasia wakati wa utawala wa kijeshi.Na hii
sio kusema eti lazima tuwakabidhi mamlaka majenerali jeshini.Badala yake,
lazima tuangalie,mifumo ya utawala wa kizamamani kabla ya kuja kwa wakoloni.
Tunaweza
kujifunza kutoka kwa mifumo hii na kubadili namna ambavyo tunatawaliwa ili
ufisadi upungue ,viwango vya umaskini vishuke na kisha ghasia pia ipungue. Mfumo
wa kisasa wa maisha umesababisha athari kuliko manufaa. Na leo ni serikali za
magharibi pamoja na makampuni ambayo ni chanzo cha vifo vya watu wetu.
Makampuni hayo ndio yanatengeza silaha na kuuza kwa mataifa yetu ambayo
yanazitumia kwa vita mfano Nigeria na kwingineko.''
No comments:
Post a Comment