Makamu wa Rais wa Kanisa la Wasabato Ulimwenguni
Mtumishi Lowell Cooper akisoma waraka wa maafikiano ya kikao hicho mara baada
ya kura kupigwa
|
Kanisa
la waadventista wasabato ulimwenguni katika kikao chake cha mwaka mwishoni mwa
mwezi uliopita, limepiga kura za kupinga uwekwaji wakfu kwa wanawake
kitendo kilichofanywa na union tatu za kanisa hilo.Union zilizopitisha hatua hiyo ni za Ujerumani
kaskazini, Columbia na Pasifiki,Union hizo zilipitisha mabadiliko hayo hivi karibuni.
Kufuatia mjadala wa masaa 3, kanisa la SDA Duniani limekuja na waraka ukizitaka union hizo kuacha
mpango wao huo na kubaki katika umoja katika kristo, kama alivyokaririwa Mch
Ted wilson akisema "focusing on the mission of the Church, uniting in
Christ, even though we will face some differences and disagreements.".
Kura 264 dhidi ya 25 zilikataa kuapisha wanawake.
Sehemu ya wajumbe wa kikao hicho
|
No comments:
Post a Comment