KIONGOZI wa Kanisa la Maombezi
la GRC na Ubungo, Dar es Salaam, Mchungaji Antony Lusekelo amewataka viongozi
wa dini na Watanzania kwa jumla, kutambua kuwa Tanzania ni bora kuliko dini
zao.
Mchungaji Lusekelo pia
aliwataka viongozi wa dini kuendeleza vita dhidi ya rushwa huku akisema watoa
rushwa na wapokeaji, wamejificha makanisani na kwenye misikiti.Alitoa kauli
hiyo jana jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na waandishi wa
habari ambapo alisema viongozi wa dini lazima lazima washiriki katika
mapambano ya rushwa bila woga.
Katika mazungumzo hayo,
mchungaji huyo pia alisema Serikali inapaswa kuwajibika kwa kutumia nguvu
zake za kisheria katika kulinda amani, huku akinyoshea kidole tukio la hivi
karibuni lililoashira kuvunja kwa amani, huku Serikali ikiwa haijachukua hatua.Alisema
hilo ni tatizo kubwa na kwamba ni watu wengi wakiwamo viongozi wa dini
kushindwa kusema ukweli kwa kuogopa maisha yao kuwa mafupi.
“Ni muhimu kila mwananchi
kutambua kuwa Tanzania ni bora kuliko Ukristo na Uislamu. Watu wengi
wanaogopa kusema ukweli. Hata viongozi wa dini kwani watoa rushwa wamejificha
misikitini na makanisani, tuendeleze mapambano dhidi ya rushwa ipo siku
tutashinda,” alisema.Kuhusu vurugu nchini, alisema
chanzo ni viongozi wa dini kuhubiri siasa za chuki misikitini na
makanisani.
“Vurugu siyo asili ya binadamu
inatengenezwa, Serikali ina wajibu wa kutumia nguvu yake kisheria kuilinda
amani na amani haishuki kutoka mbinguni au kwa maombi, inatengenezwa pia.
Tatizo cheche za kidini zilipoanza hazikudhibitiwa. Serikali ilikuwepo, aidha
kwa makusudi au bahati mbaya imelea cheche hizo,” alisema Lusekelo.
No comments:
Post a Comment