Tuesday, October 23, 2012

Kanisa la KKKT latangaza tarehe 28/10/2012 kuwa siku ya maombi ya kufunga na kuomba kuliombea Taifa



Askofu mkuu wa KKKT Askofu Malasusa

Kufuatia matukio ya Uvunjifu wa Amani unaofanywa na kikundi cha watu wachache kwa mwamvuli wa "dini". Kanisa La Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) limetoa Waraka Elekezi Wa Wachungaji Wake Wote Tanzania kuelekeza kuwa siku ya tarehe 28 October, 2012 ni siku ya Kufunga na Kuomba kwa ajili ya Amani nchini Tanzania.

Kanisa la KKKT linakuwa kanisa la Kwanza Tanzania kupitisha siku ya Kikanisa la Kufunga na Kuomba kwa ajili ya Amani Ya Nchi ilivyo Sasa.

Blog hii ambayo imefanikiwa kuutia machoni waraka huo uliotumwa na Maaskofu Dayosisi zote KKKT Wakuu wa Vituo vya Kazi za Umoja, KKKT na nakala yake kutumwa naibu Katibu Mkuu, Wasaidizi wa Maaskofu,  Dayosisi zote K,K KT, Makatibu Wakuu Dayosisi zote kuwaelekeza kwamba tarehe 28 Octoba ni Siku ya Kufunga na Kuomba. 

Waraka huo umeelekeza "Kufuatia matukio ya kuchoma Makanisa yaliyotokea hivi karibuni,barua  inawataarifu kuwa siku ya Jumapili tarehe28 Oktoba 2012 imepangwa kuwa siku maalum ya kuombea amani katika nchi yetu.Pamoja na mambo mengine yaliyokwishakupangwa kufanyika siku hiyo ( 28 Oktoba2012)' tafadhali sharika, mitaa na Vituo vya Kazi za Umoja vyote vya Kanisa letu vifanye maombi  hayo"

Kwa Mujibu wa Barua hiyo Ya Mtendani Mkuu wa Kanisa la KKKT inawataka Waumini wa Kanisa hilo kuendelea Kuhimizwa Kufunga na Kuomba Kwa Kadri Roho Wa Bwana atakavyowaongoza kuombea amani ya Tanzania. Blog ikunukuu sehemu ya mwisho ya barua hiyo inaeleza kuwa "Baada ya maombi ya siku hiyo, Washarika wahimizwe kuendelea kufunga na kuomba kadiri Roho wa Mungu atakavyowaongoza" mwisho wa kunukuu.

Ipo haja na Kanisa la Tanzania Kuungana Sambamba na Kanisa la Kiinjili La Kilutheri Tanzania katika Kuombea amani ya Tanzania.

Source:Sam Sasali

2 comments:

  1. WAKRISTO TUFUNGE TUMLILIE MUNGU ATUPIGANIE KAMA ISRAEL WALIPOINGIA KANANI WALIIMMBA TU MUNGU AKAWAPIGA ADUI ZAKE

    ReplyDelete
  2. TUSIFUNGE TU KUOMBEA WALE WANAOCHOMA MAKANISA TUFUNGE NA KUWAOMBEA WALE VIONGOZI WA DINI WENYE ROHO ZA KIFISADI WANAOCHUKUA MCHANGO YA KUJENGEA KANISA NA KUILA JEE HAWAKATISHI TAMAA WAUMINI SHETANI AMEINGIA NDANI YA KANISA VONGOZI WA DINI NAO NI MAFISADI HAWANA UPAKO NI KUENDESHA DINI KIMAZOEA TU NI SAWA NA ENZI ZA MFALME SAULI UPAKO ULIPOHAMISHIWA KWA MFALME DAUDI SIKUMBUKI IWAPO WAKATI WA MFALME SULEIMANI WALIIBA HELA ZA UJENZI WA KANISA SI LNGEKUWA LIKIJENGWA HADI LEO KUKATA ASILIMIA KUMI MCHANGO WA JENGO KANISA LA KOROGWE MBONA WANAOOCHANGIA VIFAA HAVIKATWI ASILIMIA KUMI HUU NI WIZI NDANI YA KANISA SHETANI ASHINDWE KWA JINA LA YESU

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...