Friday, October 19, 2012

Kijana atoa Ushuhuda jinsi Mungu alivyomtoa katika Ibada za Kishetani




Nilijiunga na dini ya shetani nikawa nakunywa damu na kufanya mambo mengi mabaya ambayo sikutarajia kuyafanya, niliiuza nafsi yangu kwa shetani kwa miaka 30.Huu ni sehemu ya ukiri katika ushuhuda wa kijana mfanyabiashara mwenye miaka 29 raia wa Ghana ambaye kiu yake ya kuwa tajiri ilimfikisha hapo alipo.Akiwa na miaka 21 steven Koffi(sio jina lake halisi – kwa usalama wake) kijana kutoka pwani ya magharibi nchini Ghana alijiunga na Satan international church kwa lengo la kujipatia mali.

Namna alivyojiunga na kanisa hilo

Steve alianza kusema alipokuwa mwaka wa mwisho katika chuo kikuu cha Ghana alipokuwa akisomea Masters Digrii ya nishati ya gesi na mafuta (oil and gas engineering), mambo hayakuwa mazuri kwake kifedha hivyo hakuwa na pesa ya kumalizia ada.Alipojaribu kuwaelezea wazazi wake nao pia hawakuwa na uwezo wa kumsaidia.
Steve anasema kuna mtu ambaye alikuwa akichart naye kwenye Internet na mara nyingi alikuwa akimsaidia kifedha,hivyo ilimbidi amuelezee shida yake.

Safari hii jamaa huyo alimwambia siwezi kukusaidia kwani nimekuwa nikifanya hivyo mara kwa mara sasa na wewe jitafutie pesa.Stive alishindwa kujua ajitafutie vipi ndipo jamaa huyo aliyekuwa akiishi nchini Marekani alimuelekeza Satan Chapel lilipo nchini Ghana ili steve akajiunge nalo.

Kwa kuwa Steve alikuwa na shida na alijua atapata msaada wa fedha alienda, kisha branch hiyo ya Ghana ilimtengenezea mazingira yote kuanzia pasport mpaka nauli ya yeye kwenda Califonia nchini Marekani katika shughuli ya kuingizwa rasmi katika jamii hiyo ya waabuduo shetani. Baada ya kuwa mwanachama aliomba aonane na kiongozi wa dini hiyo(Devil) ombi ambalo lilikubaliwa.Baada ya wiki mbili na alipokutana na kiongozi huyo alipewa nafasi ya kuomba mambo matatu katika maisha yake na atapewa Jambo la kwanza Stive aliomba kuwa na Mali nyingi, la pili ni kuwa Maarufu na la tatu ni kuishi maisha marefu.

Katika maombi yake yote hayo alipewa, lakini ombi la tatu lilikataliwa na Devil kwa kuwa katika sheria ya dini hiyo ni kuwa kwa yeyote atakayejiunga nao atatakiwa kuishi miaka 30 tu baada ya kujiunga na sio zaidi.Hii ina  maana kama ulijiunga na ukiwa na miaka 20 utaishi miaka 30 baada ya hapo ukiwa na miaka 50 ndipo utatakiwa ufe.Kwa kuwa Steve alikuwa na shida na pesa aliuuza utu wake kwa miaka 30 kifupi ali-likubali sharti hilo.

Wakati wa  kujiunga nao aliletewa Satanic Bible pamoja na gloves, upanga wa kiapo, suti maalumu pamoja na vingine vingi.Stive anasema baada ya kujiunga katika hatua hiyo ya awali hakupoteza uanadamu/utu wa kawaida mpaka alipojiunga na kundi lingine la juu ndipo aliongeza nyoya kwenye kofia yake.stive aliendelea kushuhudia kanisani hapo akisema nilipojiunga na kundi lingine aliamua kuitoa sadaka hali yake ya ubinadamu(manhood) na hapo ndipo mali zake zilizidi kuongezeka.

Mch Lazaro Mouka wa kanisa la Loard Choosen la nchini Nigeria alimfanyia maombi Stiven na Mungu akamuweka huru

Pamoja na mali zake kuongezeka alipewa jukumu la kuwaingiza watu wengine kwenye dini hiyo jambo ambalo alifanikiwa kwa kuwashawishi kupitia fedha alizokuwa nazo na  zaidi ya nafsi 23 ziliingia  katika imani hiyo.Stive anasema alikuwa na ofisi nchini Nigeria Katika miji ya Port-Harcourt, Warri, Abuja, na  Ghana. Steve anasema hao nliowaingiza niliwaambia nini cha kufanya kisha wakawa wanajitengenezea pesa

Kashikashi zilivyoanza

Stive Koffi anasema baada ya kutengezeza pesa za kutosha kupitia biashara ya mafuta, aliamaua kumfungulia mama yake nchini Ghana Orofa maalumu la kibiashara(PLAZA), lakini cha kushangaza mama yake ambaye alikuwa AMEOKOKA alikataa na akasema “hataki fedha zenye damu”.Mama huyo alikuwa karibu sana na  YESU na alionyeshwa kwenye MAONO chanzo cha utajiri wa mwanaye (Stive) ingawa baba yake na ndugu zake wengine walizikubali mali zake.

Kuokoka
Stive mwenye mke na mtoto mmoja alianza kukosa amani kabisa na maisha aliyokuwa akiishi, akiwa katika hali hiyo aliazimia kuwatafuta wahubiri wakubwa ili waokoe maisha yake.Taarifa zilipowafikia viongozi wa dini hiyo ya kishetani kuwa Stive anataka kuwasaliti wao waliamua kumuadhibu kwa kumpa siku 49 za kuishi baada ya hapo angekufa.Ndani ya siku hizo 49, siku ya 19 alikutana na nguvu za Mungu zilizomfungua kupitia Mch Mouka wa kanisa la Loard Choosen la nchini Nigeria.

Baada ya kupitia katika misukosuko hiyo, Stive aliwaasa vijana kanisani hapo wakati akitoa ushuhuda kuwa vijana wasiweke tamaa mbele kisha akawashauri wazazi wawe makini na vile vitu ambavyo watoto wao hupenda kuviangalia kwenye Television.Steve Koffi alimtukuza MUNGU zaidi na kusema anamshukuru Mungu kwa kuwa utu wake wa kibinadamu umerudi na anafuraha.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...