DNA
alipokuwa akiwasili nchini Tanzania mwishoni mwa wiki iliyopita
|
Denis
Kagia mwanamuziki kutoka Kenya alimaarufu kwa jina la DNA, juzi jumapili alikuwa
mmoja wa waimbaji kwenye club ya usiku ya Bilcanas iliyoko mitaa ya posta jijini
Dar es salaam.DNA alipoulizwa na waandishi wa habari akiwa ndani ya club hiyo ikiwa
ameacha wokovu ama laa yeye alijibu
“
SIJAACHA WOKOVU,BADO NIMEOKOKA LAKINI NIMEBADILI MUZIKI WANGU KWA SASA NAFANYA
MUZIKI WA KAWAIDA KAMA NILIOKUWA NIKIUFANYA.NILIOKOKA ILI NIACHANE NA POMBE, NA
NIMEWEZA NA NIKO KWENYE IMANI BADO”
Ikumbukwe
kuwa DNA aliyewahi kutamba na nyimbo ya BANJUKA, kwa sasa anatamba na nyimbo
yake isemayo “MASWALI YA POLISI”. Mwaka juzi (2010) DNA aliutangazia umma kwamba
ameokoka na kilichofuatia alianza kuimba nyimbo za injili.Kabla ya wokovu Denis
Kagia alikuwa akisumbuliwa sana na unywaji wa pombe kupita kawaida pamoja na
matumizi ya sigara.
Baada ya kuokoKa DNA pamoja
na kufanya muziki wa injili pia alikuwa mtangazaji wa kituo cha One Fm cha
nchini kenya.Nchini Kenya suala la mwanamuziki huyu kurudi kufanya circular
music lilizua gumzo katika kanisa la kenya na kila mmoja alitafsiri alivyoweza
huku wengi wakiamini jamaa ame back slide
No comments:
Post a Comment