Friday, October 19, 2012

Ephraim Sekeleti aanza maandalizi ya Muvie yake nyingine iitwayo Church Boy


Sekeleti and his Wife

Ephraim Sekeleti Mutarange mzaliwa wa Kalulushi nchini Zambia ambaye anamtumikia  Mungu nchini humo kwa njia ya uimbaji ameanza maandalizi kwa ajili ya kutoa muvie yake mpya iitwayo Church Boy.Kwa mujibu wa Sekeleti mwenyewe muvie hiyo itafanyika mwakani na kwa sasa star huyo wa “Uniongoze” na “Mungu Usiyelala” amejipanga kufanya Audition(Usaili) wa wale wote wanaoamini wana vipaji na wanataka kuwemo ndani ya Church Boy.

Usaili huu utafanyika mwezi wa kwanza mwakani huku mamia ya watu kutoka Lusaka na miji mingine wakionekana kuvutiwa na hatua hiyo.Hii itakuwa ni Muvie ya pili kutengenezwa na Sekeleti kufuatiwa muvie yake ya kwanza aliyoitengeneza mnamo mwezi wa saba mwaka huu wa 2012 iitwayo INNOCENT.Sekeleti ni mmoja kati ya wanamuziki wa Afrika wanaoiangalia Film Industry kama mkondo mwingine wa kumtangaza Kristo.

Kwa hapa nchini mwamko wa kufanya Christian Muvie nao uko juu kwani Hosanna Inc imekutana na wapendwa wengi wenye Hasira na hii Industry huku wengine tayari wameshafanya muvies zao na wengine wako chimbo.Kuna orodha ndefu ya watumishi nchini ambao wameamua kufanya Christian muvies serious wakiongozwa na Jenipher Mngendi,Emmanuel Myamba, James Temu, Bahati Bukuku,Nathan Yamungu, huku KIANGO MEDIA chini ya Samuel Sasali na living Testimony  bro Prosper Mwakitalima wakiwa nao wanajikoki.

Sekeleti katika moja ya vipande ndani ya muvie yake ya Innocent 
Big Boss The Innocent
Sekeleti ndani ya Innocent 
Innocent the Muvie 

Ephraim Church Boy

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...