Saturday, October 13, 2012

Kisima Music Awards 2012, Wanamuziki wa Injili nchini Kenya wala sahani moja na wa Secular



Tuzo za Kisima Music Awards zitolewazo nchini Kenya kwa mwaka huu zimeingia katika msimu wake wa kumi ambapo zitakuwa na Categories 12.Ikumbukwe kuwa kiushiriki tuzo za Kisima ni tofauti kabisa na Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards kwa kuwa ndani ya tuzo hizi wao huwajumuisha wanamuziki wote wakiwemo wa Gospel na Secular.Hivyo kwa kiasi kikubwa tuzo hizi zinaushindani kuliko hizi za hapa kwetu Tanzania.

Katika orodha iliyotolewa na Management ya KISIMA AWARDS inaonyesha mwaka huu kuna jumla ya kategories kumi na mbili.Kati ya hizo karibu kila kategory wanamuziki wa injili wamechomoza sambamba na wa-secular na hivyo kupelekea ushindani kuwa mkubwa.Kwa mfumo wa Gospel Music nchini Kenya ni kitu cha kawaida kuona nyimbo za wanamuziki wa injili nchini humo kupigwa kwenye vipindi vya redio za secular.Ki-bongo bongo ni kama ukute nyimbo za Bonny Mwaitege zikipigwa ndani ya XXL ya Clouds Fm na hii inatokana na wanamuziki wengi vijana wa Kenya wao wamejikita kwenye GOSPEL FLEVA.


Emmy Kosgei mmoja wa wanamuziki wa injili nchini humo na mwaka jana alikuwa ndiye mwanamuziki bora wa kike wa injili Africa na hii ni kwa mujibu wa tuzo za muziki wa  injili Barani Africa(AGMA)
Chakufurahisha ni kuwa wasanii wetu wa nchini wameweza kuchomoza  kwenye Category ya Best East East African Recognition Award ambapo imeingiza wasanii 4 kati ya saba 7 ikiwa nafasi 2 zimechukuliwa na Uganda na moja ni ya Sudan Kusini.Wanamuziki wa Tanzania walioingia wote ni wale wanaofanya secular huku kukiwa hakuna mwanamuziki wa injili nchini anayewania tuzo hizo ambazo zinaaminika kuwa ni BORA  katika Afrika Mashariki na kati.Washindi wa mwaka huu wanatarajiwa kutangazwa November 2 katika katika ukumbi wa KICC.

Hapa chini sehemu ya categories za Kisima Music Awards 2012 ambazo kwa sehemu kubwa zimekuwa na competition.

Artist of the Year
1. CampMulla
2. Nameless
3. Daddy Owen
4. Nonini
5. Octopizzo
6. Emmy Kosgei
The winner in this category will walk away with Sh2 million (US$22K)!

Best Hip Hop Artist
1. Mafans – Cannibal
2. Prep – Xtatic
3. On Top – OCTOPIZZO
4. Swahili Shakespeare – Rabbit
5. Colour Kwa Face – Nonini
6. Exponential Potential – Juliani

Anaitwa Minister Juliani, hapa aiwa na tuzo zake za kisima alizotwaa mwaka jana

Best Collabo of Year
1. Don’t Want To B Alone – Ay ft Sauti Sol
2. Make u Dance – Keko ft Madtraxx
3. Mpita Njia – Alicios ft Juliana
4. Mbona – Daddy Owen ft Denno
5. Gentleman – P Unit ft Sauti Sol
6. What You Like – Longombas ft Mr. Vegas

East African Recognition Award
1. TMK – Kichwa Kinauma (TZ)
2. Jackie Chandiru – Golddigger (UG)
3. Lady Jaydee ft. Mr Blue – Wangu (TZ)
4. Profesa_Jay – Kamiligado (TZ)
5. Chameleone – Valu Valu (UG)
6. Diamond – Mawazo (TZ)
7. Dynamq – Jere Jere (Southern Sudan)

Music Video of the Year
1. Nameless – Coming Home
2. Rabbit – Swahili Shakespeare
3. Juliani – Exponential Potential
4. Daddy Owen – Mbona
5. Nonini – Colour kwa face


Daddy Owen, tayari amesema endapo atapata tuzo hizi za Kisima 2012 atatoa 1Million  kwa ajili ya kuwasaidia watoto waishio katika mazingira magumu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...