Rais Kikwete akiangalia uharibifu uliofanywa |
Jeshi la Polisi
Mkoa wa Temeke limefanikiwa kukamata watuhumiwa wanne wanaohusishwa na
kufanya vurugu katika kituo cha Polisi Mbagala wakiwa na baadhi ya vitu
vilivyoibiwa kufutiwa uvamizi wa makanisa katika eneo la Mbagala Wilaya ya
Temeke, Jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Temeke Kamishina Msaidizi wa Polisi(ACP) David Misime aliwataja watuhumiwa hao
ni kambi Hajidi, Hamadi Salehe, Shabani Hamisi na Majebele Elias wote ni wakazi
wa Mbagala na Mtoni Mtongani.
Kamanda Misime alivitaji vitu hivyo ni komputa
moja, keybodi pamoja meza moja ndogo, vitu hivyo vyote vimetambuliwa kuwa ni
mali ya Kanisa la Kkkt Mbagala, Jijini Dar es Salaam.
Aliongeza kuwa watuhumiwa hao wote watafikishwa
mahakamani baada ya taratibu za Upelelezi kukamilika ili sheria iweze kuchukuwa
mkondo wake.
Mbali na mambo mengine amewataka wananchi kuendelea
kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa zitakazowezesha
kupatikana kwa vitu vyote vilivyoibiwa pia kutokubali kununua vitu vitu
kiholera
No comments:
Post a Comment