Friday, October 5, 2012

Rivers of Life waelekea Mombasa KihudumaRivers of Life wakiwa madhabahuni wakati wa Sifa Zivume Concert
Kundi la Rivers of Life kutoka kanisa la Dar es salaam Pentecost church(DPC) leo asubuhi limeanza safari kuelekea jiji la Mombasa kwa ajili ya kufanya huduma.Kundi hili lina  idadi kubwa ya watumishi mahiri katika uimbaji wakiwemo John Lisu, Pastor Paul Safari, John Kagaruki, Bale na wengine wengi.


Mapema leo John Lisu ameiambia HOSANNA INC kuwa safari yao ni mahususi kwa ajili ya kufanya matamasha ya kusifu na kuabudu kwa siku mbili jumamosi na jumapili hii katika kanisa la Mombasa Pentecost Church.Safari hii kihuduma inafuatia baada ya safari ya kwanza ambayo JOHN LISU pamoja na team yake walifika nchini Kenya mwezi May 2012 katika jiji la Mombasa na Nairobi na kufanya huduma ziara iliyopewa jina la JEHOVA YU HAI TOUR.

Kwa muda mrefu sasa Pastor Safari,Minister John Kagaruki pamoja na John Lisu wamekuwa wakienda nchini Kenya kihuduma na kwa sasa imekuwa ni Another Level kwa kuwa wameongozana na KIKOSI KAZI(Rivers of Life).Kwa wafuatiliaji wa mambo ya uimbaji kwa Africa Mashariki na kati ni wazi kuwa kuna viwango vya uimbaji ambavyo Mungu amekuwa AKIIPELEKA TANZANIA kila kukicha.Tunaamini Mungu atakuwa pamoja na watumishi hawa.


John Lisu na Timu yake walipouwa wakihudumu nchini Kenya wakati wa JEHOVA YU HAI TOUR

Lisu with his crew  katika JEHOVA YU HAI TOUR nchini Kenya


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...