Friday, October 19, 2012

Wananchi wateketeza kwa moto Matrekta ya Kanisa la Efatha Sumbawanga


Shamba la Malonje linalomilikiwa na Kanisa la Efatha limepata hasara kubwa baada ya wananchi wa kijiji cha Sikaungu wilayani Sumbawanga vijijini mkoani Rukwa, kujichukulia sheria mkononi na kuvamia moja ya kambi yaShamba hilo iitwayo Sikaungu na kuyateketeza kabisa matrekta mawili makubwa aina ya New Holland na kubomoa baadhi ya nyumba kwenye kambi hiyo.

Moja ya matrekta hayo

Mchungaji Kiongozi Michael Meela wa Kanisa la Efatha mkoani Rukwa akiongelea kuhusu suala hilo alisema hasara iliyopatikana ni zaidi ya shilingi milioni 228 na kwamba tukio hilo lilitokea mara tu baada ya Mbunge wa Jimbo la KwelaMh. Ignas Malocha kuhutubia mkutano wa hadahara kijijini hapo na kuwahamasisha wananchi watumie nguvu ya umma kuyakomboa mashamba yao yaliyochukuliwa na mwekezaji huyo.

Kamnda wa polisi wa mkoa wa Rukwa Bw Jacob Mwaruanda akithibitisha kuhusu sakata hilo alisema tayari wanawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kufanya uharibifu huo mkubwa na kwamba wanatarajiwa kufikishwa wakati wowote mahakamani.

Source:Tunu Bashemela

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...