Miriam Lukindo na Neema ndani ya Shilo Records |
Magwiji
wawili wa muziki wa injili nchini Miriam Lukindo Mauki pamoja na Neema mwaipopo
hivi karibuni wanatarajia kutoa Album yao ya pamoja yenye nyimbo za kusifu na
kuabudu .Album hiyo inarekodiwa katika studio ya kisasa kabisa iitwayo Shilo
Records iliyoko Boko jijini Dar es salaam chini ya producer Yohana Luhanzo.Humo
ndani kwenye keyboard yupo Paul Sagenge
na Fred Msungu, bass gitaa kasimama Emmanuel Mabisa na Chriss Mwasota kapiga
drumz.
Kwa
wachambuzi wa muziki nchini watagundua combination ya Miriam na Neema Mwaipopo
si ya kawaida kwa kuwa kila mmoja ana aina tofauti ya uimbaji hivyo
kitakachotoka hapo tunaamini kitakuwa tofauti na bora for the Kingdom Glory.
Wakati
Miriam Mauki amezoeleka kama muimbaji flani hivi ambaye toka Kitambo amekuwa
mpenzi wa Muziki wa KWAITO kabla hata watanzania hawajaukumbatia(uhusudu), pia
Miriam kwa asili ni Worshiper na hili aliwahi kulithibitisha mwenyewe wakati alipofanya
Interview na Hosanna Inc mwaka jana mwanzoni(2010).Wakati watanzania wakiwa na
picha hiyo ya Miriam, Kwa upande wa Neema Mwaipopo yeye anatazamika kama
mtumishi fulani hivi wa SHANGWE.
Drumer boy Chriss Mwasota |
Neema
japokuwa huimba nyimbo za kuabudu, most of her heat songs zimekuwa ni zile
ambazo ameimba AKIUSIFIA ufalme wa Mungu, kifupi Neema kwenye Praise ndo
amejikita zaidi, so mpaka hapo unaweza pata picha hiyo combination itacome out
na nini.Always Mungu ana-suprise zaidi ya hii itakayotoka hapo na tunaamini kwa
Neema na Miriam kufanya hii COMBINENGA
even wanamuziki wengi wa muziki wa injili nao watashirikiana.
Imezoeleka
sana kwenye muziki wa secular kwa wanamuziki wao kushirikiana katika nyimbo na
album zao, lakini kwenye gospel vitu ni tofauti unakuta mtumishi kuanzia nyimbo
ya kwanza mpaka ya mwisho kaimba mwenyewe with his or her band.Sio mbaya but
lets go beyond that york endapo kuna ulazima wa kufanya hivyo.
Sehemu ya mandhari ndani ya Shilo Records |
No comments:
Post a Comment