Thursday, October 4, 2012

Askofu Desmond Tutu atangazwa mshindi wa tuzo la Mo Ibrahim 2012


   Askofu Desmond Tutu
Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana nchini Afrika Kusini Askofu Desmond Tutu ndiye mshindi wa tuzo la mwaka huu la Mo Ibrahim ambalo humtambua  rais mstaafu katika juhudi zake za kuimarisha uongozi bora barani Afrika.

Mo Ibrahim ni Bilionea mzaliwa wa Sudan ambaye hutoa tuzo hilo kila mwaka na  akitangaza mshindi jijini Johannesburg Afrika Kusini, Ibrahim amesema wakfu wake umeridhishwa na namna Tutu amekuwa akijitahidi kuzungumzia ukweli kuhusu namna ya kuimarisha uongozi bora barani Afrika.Tuzo hilo lilianza kutolewa mwaka 2006 ambapo mshindi amekuwa akituzwa Dola Milioni 5 na kupata Dola Laki Mbili kwa muda wote wa maisha yake.

Mo Ibrahim katika hatua nyingine amesema tuzo hilo halijabadilika kutoka kwa walengwa ambao huwa ni marais waliostaafu ambao uongozi wao bora wa uongozi wakiwa mamlakani ndio huchangia wao kutuzwa.Miongoni mwa marais ambao wamewahi kushinda tuzo hilo ni pamoja na rais wa zamani wa Mozambique Joaquim Chissano , Festus Mogae wa Bostwana na Pedro Pires wa Cape Verde.Mwaka 2009 na 2010 hakuna rais aliyestaafu aliyetuzwa baada ya mshindi kutopatikana


Wa kwanza kushoto ni Bilionare Mo Ibrahim

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...