|
Mh.
Dkt. Getrude Rwakatare akiwa katika ibada hiyo |
Jumapili iliyopita Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni Mh. Dkt.
Getrude Rwakatare akitoa Ujumbe kwa Watanzania waliohudhiria Ibada Maalum ya
Kuliombea Taifa ambapo ametaka watu kutobaguana kwa misingi ya Dini, Ukabila
wala Siasa na kusema pamoja na Utawala bora pia tunahitaji maombezi ili tuweze
kufikia Malengo yaliyokusudiwa kulipeleka Taifa linapotakiwa kufikia.
Dkt. Rwakatare amesema nia kubwa ya kufanya Ibada hiyo ya Maombezi ni
kutaka kuweka usawa kutokana na siku za hivi karibuni kuibuka kwa Matamko
mbalimbali kutoka kwa watu tofauti wakiwemo viongozi wa Kitaifa, Kidini na wa
baadhi ya Makundi yanayohitilafiana na kusema tukiomba kwa jina la Mungu kila
kitu kitakwenda kama tulivyomuomba ili Tanzania iendelee kuwa nchi ya Amani na
Utulivu kama ilivyokuwa miaka yote ambayo ni kimbilio la watu wa Mataifa
mbalimbali kwa sababu Watanzania hawajui kuchukiana na wamekuwa watu wa
kushikamana kwa miaka yote.
|
Sehemu ya waumini wa kanisa hilo
|
|
Rose Muhando alihudumu madhabahuni siku hiyo
|
|
Ibada
Ikiendelea |
|
Mama akifurahia ibada hiyo
|
|
Zigizi,
Zigizi zigi,Zigizi |
No comments:
Post a Comment