Tuesday, October 2, 2012

Mhe Nabii GEORDAVIE mtumishi wa kwanza nchini kununua usafiri wa Anga(Helkopta)
Hii ndiyo Helkopta ya ya mtumishi wa Mungu Geordavie
Mtumishi wa Mungu na kiongozi wa huduma ya Ngurumo ya Upako mtumishi Mhe Nabii Geordavie mwenye makazi yake jijini Arusha,amekuwa ni mtumishi wa Kwanza nchini kumiliki usafiri wa anga kwa ajili ya kufanyia huduma.Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari mtumishi huyo anamiliki HELKOPTA na tayari anazo documents zote za umilikaji wa usafiri huo.

Nabii GeorDavie kwa sasa wengine wanamuita  MAESTRO licha ya kumiliki usafiri huo wa anga pia anamiliki kituo cha redio jijini Arusha kinachojulikana kama Ngurumo Fm Radio.Mwaka huu wa 2012 umekuwa wa baraka sana kwa mtumishi huyo ambapo siku za hivi karibuni alihitimu masomo ya THEOLOJIA kutoka chuo kimoja cha nje na kutunukiwa PHD ya Theolojia.


Nabii Geordavie Maestro akiwa ndani ya Ngurumo ya Upako Redio

Picha kwa Hisani ya Nisher (Geordavie’s son)

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...