Wednesday, October 3, 2012

I give myself a way nyimbo ilimtambulisha vizuri William McDowell

William McDowell ni mmoja kati ya watumishi wa Mungu wanaokubalika sana Duniani katika uimbaji. McDowell amekuwa maarufu sana hasa baada ya album yake ya I give myself a way kugusa mioyo ya wengi. Kabla McDowell hajaanza kuimba rasmi nyimbo zake binafsi na kuzitangaza amekuwa music Director wa Dr Ron Kenoly ambaye ni mmoja ya wakongwe wanaoheshimika sana Duniani katika uimbaji wa nyimbo za Injili.


McDowell amekuwa pia akimtumikia Mungu kama worship Pastor wa kanisa la Gathering Church ambalo linaoongozwa na  Sam Hinn mdogo wake na Benny Hinn. Katika moja ya interview zake na vyombo vya habari McDowell alisema “Mimi ni mume na baba katika familia yangu, na familia yangu ndiyo huduma yangu ya kwanza.

I give myself away ilipotoka, ilikaa kawenye chart za Billboard (gospel) kwa wiki 33. Kwa sasa McDowell anaishi Florida nchini Marekani na anamiliki studio yake binafsi iitwayo Delivery Room. Mpaka sasa wanamuziki wengi wakubwa wa injili wameshafanyia kazi zao wakiwamo  Israel Houghton Martha Munizzi, Trent Cory, Group 1 Crew, Dewayne Woods, KJ-52.

Hosanna Inc iliwahi kufanya mahojiano na Mwanamuziki wa Injili kutoka Tanzania aitwaye Miriam Lukindo na kumuuliza katika uimbaji wako unahisi wapi unafiti zaidi? Miriam alicheka kidogo kisha akasema siwezi ficha Mimi ni Worshiper. Swali hilo hilo aliulizwa Christina Shushu Mwaka jana(2011) alipoalikwa na katika kipindi cha RAUKA katika CITIZEN TV ya nchini Kenya, Shusho alisema Napenda sana kuabudu na ninapoimba nyimbo za worship nakua huru zaidi.

Swali hilo alipoulizwa McDowell alijibu “I would say that I am definitely a worshipper and that comes across in my music. I would also say that God defines what I present as a "messenger style". I am a worshipper at my core, but I do find that I deliver prophetic messages when I minister.

Kupitia Nyimbo hii ya I give myself away, McDowell alianzia Movement maalumu iitwayo “I give myself away Campaign” ikiwa na lengo la kuwasaidia mamilioni ya watu waishio kwenye mazingira magumu hususani katika kuwapatia maji safi watoto na familia kutoka sehemu mbalimbali duniani.



No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...