Monday, October 1, 2012

Word Alive Sinza waandaa Kongamano la kipekee la VijanaPastor Isaac Mallonga mmoja wa wanenaji katika kongamano hilo

Kanisa la Word Alive Sinza linaloongozwa na Askofu Deogratius Lubala lililoko Sinza Mori jijini Dar es salaam, limeandaa kongamano la kipekee la siku mbili litakalowahusisha vijana kutoka sehemu mbalimbali. Kwa mujibu wa waandaaji wa Kongamano hilo, kongamano hilo litafanyika jumamosi ijayo na jumapili (Tarehe6-7/10/2012) kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi na moja jioni ambapo chakula kitatolewa bure.Siku ya Jumapili kuanzia saa tisa mchana Kongamano litamalizika kwa IBADA KUBWA ya kusifu na kuabudu.
Kongamano hilo la vijana litakuwa likifanyika kila mwaka na kwa mwaka huu limebeba ujumbe usemao “CALL TO HIGHER DIMENSION”.Vikundi mbalimbali vya uimbaji vitahudumu vikiongozwa na Word Alive Praise Team.Kwa kijana yeyote ambaye ni mkazi wa jiji la Dar es Salaam hii si ya kukosa ukizingatia waalimu watakaohudumu Mungu ameweka hazina kubwa ndani yao kwa utukufu wa wake.Lets meet Sinza Mori jumamosi na jumapili.

wafuatao ni Waalimu watakaohudumu
1.Rose Mushi
2.Pastor Isaack Mallonga
3.Pastor Daniel Musokwa
4.Lilian Modesta Mahiga
5.Pastor Deogratius Lubala  6.Ramsey Ngwelleja    

Mwl Rose Mushi atahudumu

Pastor Daniel Musokwa mmoja wa wanenaji katika kongamano hilo
Medesta lilian Mahiga mtumishi wa Mungu na mjasiliamali naye pia atahudumu

1 comment:

  1. dada mahiga ananibariki sana na juhudi zake za ujasiliamali

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...