Friday, October 26, 2012

Ushuhuda wa mambo yaliyotokea Studio wakati wa kurekodi album ya Ingoje Ahadi ya Beatrice MuhoneBeatrice muhone

John Mtangoo ni producer maarufu sana wa nyimbo za Injili jijini Arusha, kwa muda mrefu amekuwa akijihusisha na muziki wa injili toka mwaka 1992 akiwa kama mpiga Bass kanisani.Kwa sasa John Mtangoo anamiliki studio yake jijini Arusha iitwayo CHRIST RECORD na ndiye alikuwa producer wa Album inayogusa mioyo ya wengi iitwayo INGOJE AHADI ya Beatrice muhone pamoja na Upendo Kilahiro.Hosanna Inc ikiwa jijini Arusha  ilipata nafasi ya kukaa chini na kumuuliza Mtangoo jinsi mambo yalivyokuwa tangu hatua ya kwanza ya kurekodi album hiyo.Maongezi hayo yalikuwa kama ifuatavyo.

Hosanna Inc:John wazo la kurekodi album ya Ingoje ya ahadi lilianza vipi?

John Mtangoo: Infact hili wazo la kurekodi lilikuja kama utani kwani Beatrice kwa Asili huwa anapenda sana kuimba tenzi hivyo wakati tunafanya mazoezi ya kwaya ya St James Kaloleni au kabla ya ibada nilikuwa nampigia piano Beatrice yeye anachukua tenzi anaimba.Baadaye Beatrice akaja na wazo na kusema sasa nataka kufanya Album.

Kujua kama kitu kilikuwa cha Kimungu vita ilikuwa kubwa sana,nilipokuwa natengeneza muziki nakumbuka nilifanya sequencing mpaka sa kumi alfajiri na wakati huo tulikuwa tuna-save kazi kwenye DISKATE.Ile namalizia wimbo wa mwisho diskate nayo ikafa hapo hapo hivyo product nzima ikafia hapo ikanibidi nianze upya.Haikuishia hapo wakati tunarekodi vita ilikuwa kubwa sana ilitakiwa tuombe sana nakumbuka vita ya mwisho ilikuwa ni computer,computer iligoma kufanya Mastering mpaka tuombe.

The Legendary John Mtangoo kwenye Keyboard

Fikiri nyimbo ziko kumi, unapofanya Mastering unaplay nyimbo moja moja toka dot one mpaka mwisho wa wimbo mfano wakati  Ingoje ahadi inaimba inabidi tuingie kwenye maombi wote watatu Mimi,Beatrice na Upendo Kilahiro.Ikitokea mmejikuta mmesinzia wote kwa kutegeana labda mwingine ataomba basi inakata katikati,ilikuwa lazima awepo anayeomba kwa nyimbo zote.
Achana na hiyo ya computer kugoma, kuna wakati tuko studio,mara computer ikazima ghafla pasipo tatizo lolote, hatukuwa na namna ikabidi tuipigie players BANDIKA MIKONO, KEMEA ile tu tunasema Amen computer ikawaka.Kilichotekea sasa kwa kuwa tulikuwa katika hali ya maombi so ile Anointing ya ile Album ilianzia studio.Nakumbuka wakati tunarekodi “Sarah K” alikuja studio alivyokutana na ule uwepo alivyotoka alikutana na Esther Wahome akamwambia Wahome, kuna wa-Tized(TZ) wanaimba!! Wahome akasema kuna waTz wanaweza kumzidi Mkeii(Mkenya)?

Hosanna Inc:John wakati Sarah K anaenda kuongea na Esther Wahome production ilikuwa inaendelea ?

John Mtangoo:Yeah kipindi hicho ndio tulikuwa tunamalizia kuingiza vocals, Sarah K na wahome wakachukuana walipokuja wakakuta Annointing imefunika studio kitu ambacho sitokisahau Maishani.

Hosanna Inc:Umesema wakati unarekodi alikuwepo Upendo Kirahiro, Upendo hasa alikuwa kama nani?

John Mtangoo:Upendo alikuwa rafiki wa Beatrice na ni rafiki wa Beatrice 70% ya back up alifanya Upendo na alikuwepo katika kumpa company Beatrice.

Hosanna Inc: Kuna mahali ambapo Upendo ali-lead humo ndani?

John Mtangoo:Nyimbo karibu zote Upendo naye ali lead kifupi walikuwa wanapokezana verse hii anaimba Beatrice na nyingine anaimba upendo, na ndani ya Ingoje Ahadi yenyewe verse ya pili aliimba Upendo.

Upendo Kilahiro

Hosanna Inc:John kama hali ilikuwa ndio hiyo kwa nini kwenye Album Cover anaonekana Beatrice peke yake?

John Mtangoo: Honestly Cover ya kwanza ya ile album ilikuwa na picha ya wote wawili Beatrice Muhone na Upendo Kilahiro, nafikiri kuna mahali hawakuelewana Album Cover ya pili ilikuwa na picha ya Beatrice pekee. Hayo mengine ni yao kisha Kicheko kirefuuuuu toka kwa producer huyu kitu ambacho kilinipelekea nami kucheka.

Hosanna Inc:Album iliuzwa vipi

John Mtangoo:Kabla ya kwenda kwa distributors walikuwa wanaiuza wenyewe wakitembea makanisani, Beatrice na Upendo walikuwa ni watu waliokuwa karibu sana kwa hiyo wakati wa kufanyika kwa ile kazi biashara haikuwa mbele wala hawakuwa na mikataba, hawakuwahi kuwaza huko mbele kutakuwaje walifanya kama wamoja ndicho kitu ambacho naweza kukumbuka, gharama karibu zote za utengenezaji wa album ile zilitolewa na Beatrice.

Hii ndiyo album ya Ingoje Ahadi naamini Karibu kila familia ya wapendwa ilikuwepo au bado ipo

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...