Khaya Mthethwa akiwa stejini |
•Awa mweusi wa kwanza kushinda katika shindano hilo toka
lianzishwe mwaka 2002.
•Apata randi 1m sawa na
shilingi za kitanzania 188,347,073.37na record deal
•Unabii wa Pastor Ucheagu(My god id good ooh) kuwa nchi ya south
Afrika isubiri mambo makubwa kutoka kwa Khaya wakumbukwa.
Khaya Mthethwa kijana kutoka kundi la Joyous
celebration siku ya jana alitawazwa rasmi kuwa mshindi wa shindano la vipaji
vya kuimba nchini Africa ya kusini maarufu kama South africa Idol series 8.Khaya
mwenye miaka 25 ni mweusi wa kwanza kuchukua tuzo hiyo toka mashindano hayo
yaanze mwaka 2002.Khaya mkazi wa Durban alikuwa akichuana kwa ukaribu kabisa na
binti wa kizungu mwenye miaka 23 aitwaye Melissa.
Licha ya support kubwa aliyokuwa akiipata kutoka
kwenye kundi lake la Joyous, umaridadi wake wa kuimba pamoja na kupiga kinanda
kwa umahiri vilikuwa ni vitu vilivyombeba Khaya katika mashindano hayo.Haikuwa
rahisi kwa Khaya kushinda kwani ushindani ulikuwa mkubwa, katika hatua
iliyoonekana wazi kuwa raia weusi wa Africa ya kusini wanamkubali Khaya, wengi
wao iliwabidi wanunue kadi mbili mbili ilimradi tu wampigie kura nyingi.
Khaya Mthethwa akiwajibika jukwaani |
Ikumbukwe kuwa kura zilikuwa zikipigwa kupitia
channel za kulipia(subscription chanels) ambazo kimsingi inakubidi ununue kadi
za kukuwezesha kuona na ku-vote. Kwa upande mwingine upigaji huu wa kura
uliwapelekea wengi wa mashabiki wa Khaya hususani wenye kipato cha chini
kushindwa kupiga kura.Wakati wa mashindano hayo Khaya aliwahi imba nyimbo ya Nick Minaji - Super Bass
Khaya Mthethwa akiwa na mpinzani wake Mellisa
wakati wa mchujo |
Kwa ushindi huo Khaya ameondoka na kiasi cha randi R1m ambazo ni sawa na Paundi £74,139 zenye thamani ya
kiasi cha shilingi za Kitanzania 188,347,073.37.Khaya
ambaye ameanza kuonekana na kundi la Joyous Celebration katika album yao ya 15
na kumi 16, aliwahi pewa neno la Kinabii na mwanamuziki mwezie Pastor Ucheagu
kuwa nchi ya south Afrika isubiri mambo makubwa kutoka kwa Khaya.Wengi wa wana-joyous
na ex-joyous akiwemo Nthokozo wamempongeza Khaya kwa mafanikio haya.
Khaya Mthethwa akiwa na Mnthunzi Namba katika Joyous 15 |
Kwa mujibu wa website ya Khaya,
klhaya alianza kupiga drums akiwa na umri wa miaka kumi na hii ilikuwa ni kati
ya mwaka 2001-2003 kiasha akaamua kwenda kwenye chuo cha kufundisha Sauti(Vocal
training).Tofauti na kupiga drums, Khaya ni mahiri katika kupiga gitaa,na
keyboard pia ni worshiper ,song writter na music director katika kanisa
analoabudia.
Chukua hii:Kwa Tanzania Praise leader
wenu akishiriki BONGO STARSEACH usishangae akitengwa.
No comments:
Post a Comment