Wednesday, February 22, 2012

Sio Sahihi Kuuhusisha moja kwa moja unabii wa TB Joshua na Uhai wa Rais Mugabe


Prophet Temitope Balogun Joshua
Mwanzoni mwa mwezi huu Nabii wa Mungu kutoka nchini Nigeria Temitope Balogun Joshua(TB JOSHUA)alitabiri kuwa kiongozi mmoja wa Afrika aliyedumu kwa muda mrefu madarakani ataaga dunia ndani ya siku 60 zijazo, baada ya utabiri huo kumekuwa na kauli nyingi zikiongelea utabiri huo huku wananchi wengi wa Zimbabwe wakiwa ni kwanza kuuvalia njuga utabiri huo kwa kuamini kuwa aliyekuwa akisemwa ni Rais wao yaani Robert Mugabe.

Maneno na mijadala mingi baina ya wazimbabwe ilipelekea sehemu kubwa ya Afrika na watu wasioujua ukweli wa utabiri huo kuamini wazi kuwa aliyekuwa akisemwa ni Mzee Mugabe, na hii ni kutokana na Umri wake kuwa umeenda ukilinganisha na viongozi wengine yeyote walioko madarakani katika bara la Afrika. Msemaji wa chama Tawala cha nchini Zimbabwe(ZANU PF) Mh Rugare Gumbo yeye alipoulizwa juu ya utabiri huo alisema “I do not believe some of these prophecies of doom,”

Ikumbukwe kuwa wakati Mtumishi TB JOSHUA akitoa utabiri huo hakusema ni nchi gani wala ni Rais gani japokuwa Mungu alimwambia juu ya hayo na yeye aliwaomba washirika wake wamuombee Rais huyo. Rais Mugabe sio kiongozi pekee aliyeko madarakani ambaye umri wake umeenda, wapo wengi lakini kwa nini kila mtu aliyesikia unabii huu wa Tb Joshua anaamini muhusika ni Mugabe? hilo ni swali ambalo kila mtu mwenye ufahamu angepaswa kujiuliza.

Kutokana na afya yake kuwa sio nzuri kuna kipindi Rais Mugabe kupata msaada wa walinzi wake pindi awapo katika shughuli zake
Ki umri kwa sasa Mugabe anamiaka ipatayo 88,baadhi ya Marais wengine wa Afrika wenye umri mkubwa ni pamoja na Rais wa Senegal Mh Abdoulaye Wade mwenye miaka 85 ambaye anaheshimika sana kisiasa kwa kuwa upande wa upinzani kwa miaka ipatayo ishirini kabla hajaingia madarakani. Mwingine ni Rais wa Kenya Mh Mwai Kibaki mwenye umri wa miaka 81.

katika orodha hii ya wakongwe yumo pia Rais wa Cameroon Mh Paul Biya mwenye umri wa miaka 79, Rais Biya yeye amekuwa kwenye uongozi kwa takribani miongo mitatu na bado hajaonyesha nia ya kuachia madaraka wakati Rais mpya wa Sadc Mh Michael Sata wa Zambia yeye anaumri wa miaka 79 na kwa muda sasa  na ameripotiwa kusumbuliwa na maradhi mbalimbali. Nchini Malawi wamalawi nao wanamuhusisha Rais mkongwe wa nchi hiyo Mh Bingu Mutharika(79) katika kundi hilo na unabii wa Tb Joshua.

Wakati Nabii wa Bwana TB Joshua akitoa unabii huo kanisani kwake alisema na hapa ninamnukuu “We should pray for one African head of state, president against sickness that will likely take life. It is sickness for a long time – being kept in the body for a long time (sic).“God showed me the country and the place but I’m not here to say anything like that. I am still praying to God to deliver the president concerned.”

Swali linarudi kwa nini Mugabe?, kila kona Mugabe? Hili linabaki kuwa ni fumbo japokuwa wengi wanauhusisha unabii huo na afya ya Mugabe ambapo mara kwa mara imeripotiwa kuwa sio nzuri, lakini ukweli unabaki pale pale wengi wa wakongwe hao hapo juu afya zao sio nzuri.

Kibiblia unabii utokao kwa Mungu ni lazima utimie(it shall come to pass), Mungu anabaki kuwa Mungu na hulithibitisha lile alisemalo toka Enzi na Enzi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...