Thursday, February 9, 2012

Friends on Friday MbeyaUle usiku unaowakutanisha watu mbalimbali hususani waliookoka kwa lengo la kukaa pamoja kula, kunywa,kuimba, kucheza kupitia live band(Gospel)na pia  kubadilishana mawazo,utaalamu,na kuapdate minds kifupi kuongeza Network kwa utukufu wa Mungu.Friends on Friday itafanyika kwa mara nyingine jijini Mbeya katika ukumbi wa Metro Cuisine siku ya tarehe 24/02/2012.

Friends on Friday ambayo kimsingi ilianzia jijini Dar es salaam na sasa imefika jijini mbeya na hapo baadaye itasambaa katika mikoa mingine hususani Arusha na Mwanza. segments zilizomo ndani ya tukio hilo ikiwamo Motivation Talks huamsha hisia na morali kwa wahudhuriaji kuweza kubadilika kimtazamo na pia kuchangamkia fursa zilizopo kwa maendeleo ya nchi na kanisa kwa ujumla.
No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...