Boaz Sollo |
Mtumishi wa Mungu Boaz Sollo kwa sasa amekuwa akisikika sana katika masikio ya watanzania hususani walio karibu na Media, mchungaji Sollo ni kiongozi wa kanisa la lijulikanalo kama EndTime Harvest Church lenye makazi yake mkoani Iringa. Amekuwa akihubiri injili katika sehemu mbali mbali na hivi karibuni alifanya mkutano wa injili mkoani Dodoma.
Mchungaji Sollo alimpokea Yesu kama Bwana na mwokozi wa Maisha yake mnamo mwaka 1997 na baada ya kuukulia wokovu amekuwa akifundisha na kuhubiri sehemu mbali mbali nje na ndani ya Tanzania. Kwa upande wa elimu Mch Sollo ni Mhitimu wa shahada ya Theolojia katika chuo kikuu cha Breakthrough Bible College kilichoko nchini Marekani.
Mungu amekuwa akimtumia Mch Sollo kwa ishara kubwa na maajabu ambapo katika mikutano yake na Ibada kanisani kwake watu wengi wamefunguliwa kwa uweza wa Mungu.Tofauti na kuhubiri Mchungaji Sollo ni ni mwandishi na Muimbaji wa nyimbo za injili ambapo mpaka sasa amesharekodi jumla ya Album za muziki wa injili zipatazo tatu.
No comments:
Post a Comment