Saturday, February 11, 2012

Wakenya Waandaa Filamu ya Yesu Kwa Viwango vya PremieresWalking with Jesus ni Filamu  inayotayarishwa nchini Kenya inayoonyesha Maisha ya YESU Kristo katika Mazingira ya Kiafrika. Filamu hii imechukua mtitririko wa Matukio mbalimbali ya Maisha ya YESU kutoka katika Filamu za YESU zilizotangulia Zile za zamani na zilizotoka miaka ya hivi karibuni.Kwqamujibu wa waandaaji wa Filamu hiyo ,Filamu hiyo itakuwa ni ya Viwango vya juu kabisa yaani PRIMIERES.

Walking with Jesus pamoja na kuonyesha mambo ya zamani Pia imeelezea mbinu za kisasa za kuweza kuhubiri Injili ya YESU KRISTO. Video hii imetengenezwa na waafrika kwa na kuigizwa na waigizaji kutoka nchini Kenya ambapo Location ya Video nzima ilifanyikia nchini Kenya huku Lugha iliyotumika ikiwa ni Kiingereza

Hapa nchini Tanzania vimekuwepo vikundi mbalimbali na taasisi mbalimbali ambazo zimewahi kuigiza Filamu ya Yesu kwa Lugha ya Kiswahili. Changamoto kubwa ni Ubora wa Video hizo kwa kuwa zinachukua muda mfupi kutayarishwa huku viwango vya teknolojia vilivyotumika kuwa duni.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...