Thursday, February 9, 2012

Mch Anthony Lusekelo Apinga Vikali Mgomo wa Madaktari


Mch Anthony Lusekelo

Mch Anthony Lusekelo wa kanisa la GRC Ubungo jana tarehe 9/10/2011 kupitia Kipindi chake cha TUTASHINDA kinachoonyeshwa na kituo cha Television cha Chanel Ten alitoa msimamo wake juu ya mgogoro unafukuta hivi sasa nchini baina ya madaktari na serikali ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Mch Lusekelo apinga vikali kitendo cha madaktari kuwaacha watanzania wanateseka kisha wao wanakaa pembeni kisa wanadai ongezeko la posho na mazingira bora ya kufanyia kazi.

Mtumishi Lusekelo aliwasihi madaktari waliogoma warudi wodini kufanya kazi zao kwa kuwa wodi kwao ndio MADHABAHU yao hivyo warudi madhabahuni. Mtumishi huyo alienda mbali zaidi na kusema wanachokifaya madaktari hao ni zaidi ya ufisadi wa Nyamongo  kwa kuwa Ufisadi wenyewe  huua watu taratibu(polepole) wakati wanachokifanya wataalamu hao ni kuua watu kwa haraka zaidi kwa kuwa mtu anakufa unamuona ndani ya muda mfupi.

Akasema Kibiblia Kugoma ni jambo Haramu, na pia Biblia inasema Usiue hawa jamaa wanaua watanzania wenzetu wenye hali duni. Katika mahojiano hayo Mt Lusekelo alisema Serikali inapaswa kuchukua rekodi ya wote walioingia kwenye mgomo huo na kutopewa heshima yeyote kwenye rekodi ya nchi hii.Aliipongeza Serikali kwa juhudi zake za kukubali kukaa na madaktari na kufikia muafaka japokuwa madaktari hao waliendelea kugoma.

Aliendelea kusema hawa madaktari wao wanadai posho kama wabunge, wanataka mishahara iongezwe  na wengine wao nwanataka mshahara iongezwe mpaka kufikia Milion 17 kwa mwezi!!!. Kisa cha yote haya eti kwa sababu ya unyeti wa kazi yao ya udaktari, akasema hapa nchini kila anayefanya kazi anao umuhimu wake, leo hii majambazi yakipora na kuiba daktari haendi ila Polisi ndio wanahusika, hivyo nao wanaumuhimu wao na sio wao pekee.

Mzee wa Upako kama ajulikanavyo kwa wengi aliendelea kusema “ ukifanikiwa kuwaona hao madaktari wanajeuri kweli!!! Wanasema Hatuingii wodini,hilo pepo lililokuvagaa na kusema hauingii wodini na lile pepo linalowavaa watu wakaue albino ni sawa”. Akazidi kusema kwetu sisi wanyakyusa kumgomea mgonjwa ni kitu haramu hivyo madaktari warudi kazini huku madai yao yakisikilizwa.

Suala la migomo limekuwa tata sana hususani kwa watu waliookoka eidha wajiunge kwenye mgomo ama la huku viongozi wa dini wakiwa kimya. Kwa mara kadhaa Mwl Christopher Mwakasege amekuwa akipinga Vikali Migomo ya aina yeyote hususani ya wanafunzi vyuoni akisema mnapogoma mnamaanisha MUNGU hawezi kuwapa majibu bali huyo mnayemgomea ndio mwenye jibu juu ya tatizo lenu.

Hii ni wiki ya tatu sasa mgogoro kati ya serikali na madaktari unaendelea na siku ya jana naibu spika Mh Job Ndungai alikubali hoja binafsi ya mbunge wa Kigoma mjini ya kuahirisha shughuli nyingine za Bunge na bunge kukaa kuliongelea suala la mgomo huo kwa kina. Awali hoja hiyo ilikuwa imewakilishwa na wabunge wengine wapatao watano lakini haikuweza kukubaliwa na aliposimama Mbunge huyo akawa wa sita ndipo ikawa kero kwa Viongozi hao wa bunge hivyo ikakubaliwa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...